BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IRAN YAFANYA MAJARIBIO KOMBORA LA KHORRAM-SHAHR, LINA UWEZO WA KWENDA MASAFA YA KILOMETA 2,000.

Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.

Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa.

Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000.

Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo.

Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo. Rais Donald Trump na rais Rouhani wa Iran

Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: