BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE ZA KIVITA ZA MAREKANI ZAPAA PWANI YA KOREA KUSKAZINI KAMA KUONYESHA UBABE

Ndege za kijeshi za Marekani zimepaa karibu na pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini katika kuonyesha ubabe wa kivita, idara ya ulinzi nchini Marekani pentagon imesema.

''Hatua hiyo ni kuonyesha kuwa rais Trump ana njia tofauti za kijeshi kushinda vitisho vyovyote'' , msemaji Dana White alisema.

Marekani na Korea Kaskazini zimerushiana cheche za maneneo katika kipindi cha hivi majuzi.

Katika Umoja wa mataifa siku ya Jumanne, bwana Trump alisema kuwa ataiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujitetea na washirika wake.

''Hili ni eneo ambalo jeshi lolote halifai kupitia na ni ndege za kijeshi za Marekani ambazo zimeweza kulifikia katika karne ya 21, licha ya tabia mbaya ya Korea Kaskazini'', alisema Bi White.

Tangazo hili lilijiri muda mfupi kabla ya waziri wa kigeni wa Korea Kaskazini kutoa hotuba yake katika umoja wa mataifa .

Mapema siku ya Jumamosi , tetemeko lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher lilisikika karibu na kituo cha kujaribia makombora cha Korea Kaskazini na kuzua hofu kwamba taifa hilo huenda lilitekeleza jaribio jingine la kombora lake.

Lakini wataalam wamesema kuwa lilikuwa tetemeko la ardhi.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: