BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SUGU ALIKULUPUA LA KWAKE NA MAMA WATOTO WAKE, NI KAMA LILE LA DIAMOND PLATNUMZ NA HAMISA MABETO

Diamond na Hamisa.

WAKATI ishu ya Diamond ikizidi kukiki kwa staili ya namna yake, huku nako balaa lingine limewaka kwa Mwanamuziki Joseph Mbilinyi “Sugu” pamoja na mama wa mtoto wake mmoja Faiza Ally.

Katika mtandao wa Instagram Faiza alimtuhumu Sugu kuwa ni baba asiyewajibika vilivyo katika malezi ya mtoto wao na kwamba Diamond amefanya wanaume wengi kama Sugu kuwadhalilisha kwa kutokuwa tayari kuhudumia familia zao.

Baada ya tuhuma hizo naye Sugu kupitia akaunti yake ya Instagram alifunguka kujibu shutuma hizo kwa kuweka picha inayoonesha risiti za malipo ambayo anayafanya kwa mtoto wake katika shule anayosoma na kudai kuwa Faiza alimkataza kulipa ada kwa kumwambia kuwa anajiweza mwenyewe. 


“Huwa sipendi kuposti mambo haya lakini imenibidi, hizi ni bank slips za ada ya mwisho niliyolipa kwenye shule ya kindergarten aliyokuwa anasoma mwanangu za mwezi wa 5 mwaka huu 2017 ambako alishamaliza.

Na mwezi huu wa 9 ilikuwa nimuanzishe Shule ya Feza Nursery pale Mikocheni, lakini from no where mama yake ghafla akanizuia na kusema ahitaji tena nilipe ada na hata kunizuia nisimuone tena Sasha! 

Na kwamba ana uwezo wa kumpeleka shule anayotaka yeye na ndio akampeleka huko Hazina International, ambako pia hata hivyo nilishaanza kuwasiliana na uongozi ili niendelee tu kulipa ada hata kama nimepigwa marufuku kumuona mwanangu bila sababu.

Hivi kama ni nyie mngefanyaje? Na nyie mnaotukana ovyo mitandaoni bila kuwa na ukweli mnaoujua tafadhali sana naomba hebu kwanza KABILIANENI NA HALI ZENU kwenye maisha... Asanteni,” aliandika Sugu.Mwananchi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: