BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WEMA SEPETU AMFARIJI LULU ANAYEKABILIWA NA KESI YA KUMUUA KANUMBA


Dar es Salaam. Msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Wema Sepetu ni miongoni mwa watu waliomfariji Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia iliyoanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Wasanii wametumia mtandao wa Instagram kumfariji mwigizaji Lulu ambaye ni mshindi wa tuzo za filamu za AMVCA.

Jackline Wopler, Katarina Karatu, Nisha, Aunt Ezekiel na wengine wametuma picha za mwigizaji huyo zikiambatana na maneno ya kumfariji wakimweleza kuwa atavuka salama katika mtihani huo.

Kupitia ukura wake wa Instagram, Wema ameweka picha ya Lulu na kuandika, “This Too Shall Pass Baby… God is Great u know… so have faith… ur in my prayers,” akiwa na maana hata hili litapita, Mungu ni mkubwa hivyo anatakiwa kuwa na imani na atamwombea. 


Lulu anadaiwa Aprili 7,2012 alimuua bila ya kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Kesi inasikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: