BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MADEREVA WALEVI SASA KUPEWA ADHABU YA KUFANYA KAZI KATIKA CHUMBA CHA MAITI

Mamlaka ya usalama wa uchukuzi nchini Kenya NTSA imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi.

Madereva walevi sasa watalazimika kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za barabarani.

''Hatuwezi kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya ajali na wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha kutengeza sera hiyo mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria'', alisema mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Meja.

Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: