BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WASIOFAHAMIKA WAHARIBU MAKUSUDI GARI, MUZIKI WA CHADEMA DAR ES SALAAM


Dar es Salaam. Watu wasiofahamika wamevamia na kuvunja vifaa vya muziki vilivyopangwa kutumika katika mkutano wa kampeni za udiwani wa Kata ya Mbweni wilayani Kinondoni.

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akiwa pamoja na Mbunge , Tarime Vijijini John Heche na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ameliambia gazeti hili Novemba 24, 2017 kuwa tukio hilo lilitokea saa 9 alasiri katika uwanja wa Mbweni Vijijini.

Jacob ambaye pia ni diwani wa Kata ya Ubungo, amesema wakati watu wakiwa pembeni wakisubiri viongozi na wanachama kufika eneo hilo ghafla lililotekea gari ndogo lililobeba vijana hao ambao walishuka na kufanya uharibifu huo.

“Walivunja muziki wote uliokuwa uwanjani kisha kuvunja kioo cha gari la matangazo lililokuwa likitumika kuhamasisha watu kuhudhuria mkutano huu,” amesema Jacob. 


Amesema hadi sasa bado hawajawatambua watu hao ambao wamefanya uharibifu huo na kwamba, hali ya utulivu imerejea katika eneo baada ya polisi kuwasili na wakati wowote mkutano utaanza wa kumnadi mgombea wao.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: