BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZANZIBAR HEROES YAIDUWAZA UGANDA MICHUANO YA CECAFA 2017 KWA KUTINGA FAINALI KENYA


Nahodha wa Zanzibar Suleiman KassimNahodha wa Zanzibar Suleiman Kassim 

Zanzibar wamefuzu kwa fainali ya ubingwa wa kanda ya Afrika mashariki na kati, maarufu kama Cecafa Senior Challenge baada ya kuwalaza Uganda Cranes 2-1.

Zanzibar Heroes sasa watakutana na Kenya kwenye fainali Jumapili.

Zanzibar walifunga mwanzo kupitia Abdul Azizi Makame dakika ya 25 kisha Derrick Nsibambi akatuliza kimiyani bao la Uganda la kusawazisha naye Mohammed Issa Juma akapachika wavuni bao la pili la Zanzibar .

Ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kufika fainali michuano hiyo tangu 1995, mwaka ambao walitwaa ubingwa.

Wenyeji Kenya walifuzu baada ya kuwashinda Burundi kwa bao la muda wa ziada lililofungwa na kiungo wa kati Whyvonne Isuza.

Katibu mtendaji wa baraza la taifa la michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee tayari amesema: "Sasa Fifa wapende wasipende watatutambua."

Zanzibar si wanachama wa Fifa licha ya kupigana kwa muda mrefu watambuliwe.

Wanajumuishwa wote pamoja na Tanzania bara, Lakini Ali asema ndugu mkubwa hawapi fungu lao kutoka Fifa.

"Nitasema hapo tumefinywa lakini tutafanikiwa siku moja."

CAF pia haitambui chama cha kandanda cha Zanzibar.

"Walijaribu kutuzuia CAF tusishiriki michuano hii ya Cecafa lakini ndugu mkubwa akatutetea tena tuliwaambia sisi ni baadhi ya waanzilishi miaka hiyo ikiwa Gossage Cup," asema Ali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: