BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DIEGO MARADONA AMTUSI RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP KWA KUMUITA KIKARAGOSI

Nyota wa zamani wa soka nchini Argentina Diego Maradona amenyimwa kibali cha kuingia nchini Marekani baada ya kudaiwa 'kumtusi' rais Donald Trump katika runinga.

Maradona alitarajiwa kusafiri kuelekea Miami kushiriki katika kusikilizwa kwa kesi ya mkewe wa zamani .

Lakini Maradona ambaye anasimamia klabu ya UAE ya Al Fujairah amekatazwa visa kwa mara nyengine kuingia Marekani.

Katika mahojiano Maradona anadaiwa kumuita Trump 'Chirolita'.

Neno hilo ni tusi linalojulikana sana nchini Argentina likimaanisha watu ambao ni vikaragosi.

Wakili wa Mardona Matias Morla sasa atamwakilisha mtaja wake katika kesi hiyo mjini Miami.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: