BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KENYA YAMSHIKILIA MTANZANIA AKITOROSHA DHAHABU UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA


Maafisa wa forodha nchini Kenya wamemkamata mwanamume anayedaiwa kuwa raia wa Tanzania katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi akisafirisha dhahabu ya thamani ya dola milioni moja, taarifa zinasema.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 46 anadaiwa kuwasili kutoka Mwanza, Tanzania kupitia uwanja wa Kilimanjaro na alikuwa safarini kuelekea Dubai.

Gazeti la kibinafsi ya Nation linasema mwanamume huyo, ambaye jina lake halijafichuliwa kufikia sasa, aliwasili uwanja wa JKIA Ijumaa 16 Februari akiabiri ndege ya Precisio Airlines na alitaka kuabiri ndege ya Kenya Airways kuelekea Dubai.

Maafisa wa uIdara ya Uchunguzi wa Jinai wakiandamana na maafisa wa uchunguzi kutoka Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) walimhoji na akaandikisha taarifa.
Kwa nini akakamatwa?

Sheria za Usimamizi wa Forodha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za mwaka 2004, kKifungu 85(3) na Kiambatisho cha Pili Sehemu B (4) huharamisha usafirishaji wa madini ambayo hayajapitia viwandani katika kanda ya Afrika Mashariki.

Vipande hivyo vya dhahabu vya uzani wa kilo 32.3 vinashikiliwa na maafisa wa idara ya forodha wa KRA huku uchunguzi zaidi ukiendelea.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: