BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Mwandishi wa Raia Mwema avamiwa na kundi kubwa la Polisi nyumbani kwake saa 9 alfajiri, na kuondoka naye

 
Kundi kubwa la Askari Polisi Wamevamia na kupekua nyumbani kwa Mwandishi wa habari wa Raia Mwema, Emmanuel Kibiki kuanzia saa 6 usiku hadi 9 alfajiri na baadaye kuondoka naye.

Mwandishi huyo amekuwa akifanya kazi zake mjini Makambako Njombe, alivamiwa na askari hao ambao idadi yao haikajulikana na kulazimisha kuingia ndani kufanya upekuzi.

Habari zilizothibitishwa na Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Ezekiel Kamwaga zinaeleza, mwandishi huyo alizuia askari hao kuingia na kufanya upekuzi bila kufuata taratibu.

Anaeleza: Nimepigiwa simu na mkewe, Tobina akilia machozi kuwa mumewe alifuatwa na askari hao majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo.

"Tulikuwa tumelala mara tukasikia mlango unagongwa. Kufungua tukaona ni askari polisi waliokuja na magari mawili. walikuwa ni askari wengi mpaka ilitisha. Sikuwahesabu lakini walikuwa wengi.

"Wakasema wanataka kupekua ndani. Mume wangu akawagomea. Akawauliza kama wana kibali cha kumpekua. Hawakuwa nacho. Kibiki anasoma masomo ya sheria kwa sasa na alishindana nao kwa hoja na Ikawa rabsha mpaka akaja mjumbe wa serikali ya mtaa. Polisi wakaruhusiwa kumpekua kuanzia saa sita mpaka saa tisa.

"Walisema wamepata maelekezo kutoka juu na kosa lake ni kwamba anaandika sana mambo ya siasa na waliowatuma hawapendi. Wamemchukua tangu saa tisa usiku na hajarejea mpaka muda huu," Tobina amenieleza kwa kilio cha kwikwi muda mchache uliopita.

Tobina na mumewe wanaishi Makambako Mjini katika eneo la Mwembetogwa. Kibiki ni mwandishi wa habari wa muda mrefu na hujulikana pia kwa lakabu (jina la utani) ya Yo Man. .

Amekuwa akiandika mawazo yake katika mitandao ya kijamii na magazeti mbalimbali likiwamo Raia Mwema/www.jamiiforums.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: