BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MHARIRI GAZETI LA GUARDIAN AOKOTWA AKIWA HAJITAMBUI BUNJU DAR


Mmoja wa wahariri waandamizi wa gazeti la The Guardian, Finnigan Simbeye ameokotwa eneo la Bunju wilayani Kinondoni akiwa hajitambui.

Taarifa zilizosambaa leo Jumapili Aprili 8, 2018 kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kitambulisho chake cha kazi cha kampuni ya The Guardian Limited zinaeleza Simbeye aliokotwa akiwa kwenye hali mbaya.

Hata hivyo, kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne alipotafutwa na MCL Digital amesema hana taarifa za tukio la kuokotwa Simbeye.

Rose Mirondo, ambaye ni mkewe Simbeye amesema mumewe aliondoka nyumbani jana Jumamosi Aprili 7, 2018 akiwa na gari lakini hakurudi hadi alipopata taarifa za kuokotwa kwake leo.

Amesema alipokwenda eneo la tukio Bunju hakuliona gari wa mumewe.

Rose amesema watu aliowakuta eneo la tukio wamemweleza kwamba Simbeye alichukuliwa na polisi kupelekwa hospitali. Amesema bado hana taarifa ya hospitali gani amepelekwa na kwamba, anakwenda Kituo cha Polisi Bunju kupata taarifa zaidi.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: