
Wakisoma hotuba zao jana Mei 3 katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Vyombo vya habari kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania, (Misa- Tan) Salome Kitomari amesema ni muhimu hatua zichukuliwe kukabiliana na hali iliyopo sasa.
Kitomari amesema, takwimu za taasisi kama waandishi wasio na mipaka na kamati ya kulinda waandishi wa habari zinaonesha kushuka viwango vya uhuru wa habari na kujieleza Tanzania.
"Lakini pia matukio ya utekwaji nyara na viwango vya unyanyasaji wa wanahabari duniani vimeongezeka sana"amesema.
Amesema mwaka jana zimeripotiwa kesi za kupotea kwa waandishi wa habari, manyanyaso na ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari.
“Leo ni siku ya 163 tangu kupotea kwa mwandishi wa habari wa Mwananchi, hakuna hata fununu tu yupo wapi ama yupo hao ni jambo ambalo linatia doa nchi yetu,"amesema
Amesema wahabari wanaitaka Serikali kupitia jeshi la polisi kuwatafuta waliohusika na kitendo hicho na kuwachukulia hatua za kisheria.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, (TEF) Deodatus Balile amesema mazingira ya kazi ya kuandika habari yamekuwa magumu kutokana na baadhi ya watendaji wa vyombo vya dola kubugudhi na kuwafanyia uonevu wanahabari, huku kukiibuka kundi la watu wasiojulikana.Mwananchi
0 comments:
Post a Comment