BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Mbunge wa CCM atakayepinga bajeti Wizara ya Mifugo na Uvuvi, apewe mshahara wangu


Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea Dodoma. 



Dodoma. Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameuweka rehani mshahara wake wa ubunge wa Mei, 2018 akitaka apatiwe mbunge wa CCM atakayesimama na kupinga bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mwaka 2018/19, inayotarajiwa kupitishwa jana Ijumaa jioni Mei 18, 2018.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti hiyo , kubainisha kuwa wabunge wa CCM wamekuwa wakipitisha kwa nguvu bajeti baada ya kuitwa kwenye vikao vya ndani vya chama hicho.

Baada ya Kubenea kueleza hayo, baadaye Spika wa Bunge, Job ndugai aliwatangazia wabunge wa chama hicho tawala kuwa watakuwa na kikao cha ndani kitakachofanyika katika ukumbi wa White House, kabla ya kurejea tena bungeni saa 10 jioni.

Mara nyingi hoja za wabunge zinapokuwa moto bungeni kuhusu wizara fulani, CCM huitisha vikao hivyo vya ndani.

“Mheshimiwa Spika kama atasimama mbunge yeyote wa CCM na kutaka kukwamisha bajeti hii, natangaza mshahara wangu wa mwezi huu apewe akaongezee bajeti yake, huwa mnatupiga maneno tu bila vitendo,” amesema Kubenea. 


Amesema ni aibu kwa Serikali kuendelea kuagiza nyama, kuku na samaki kutoka nje ya nchi wakati vitu hivyo vimejaa nchini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: