BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWENYEKITI KAMATI YA UONGOZI CUF AMTOLEA UVIVU MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU GERSON MSIGWA


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Waziri Mkuu wa zamani, Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM (NEC).

Hata hivyo taarifa hiyo iliyotumwa saa nane usiku wa kuamkia leo Mei 25, na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ilizua mjadala kwa baadhi ya wanasiasa na wadau wa masuala ya siasa kuhoji mamlaka ya Msemaji wa Ikulu na yale ya Ofisi ya Itikadi na Uenezi ya CCM.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif, Julius Mtatiro, amesema kitendo cha Msemaji wa Ikulu (Mtumishi wa Serikali) kutangaza vikao vya CCM na uteuzi wa wajumbe wa vikao vya CCM ni hatari. 


“Watanzania wanalazimishwa kukubali kuwa watumishi wa Serikali ni watumishi wa CCM. CCM ina msemaji wake lakini mambo ya CCM yanatangazwa na Ikulu.” amesema.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: