BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YATARAJIA KUWANYONGA WANAWAKE 40 HADI KUFA


Aliyekuwa rais wa Iraq. Sadamu Hussein alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.


Baghdad, Iraq. Serikali inatarajia kuwanyonga wachumba 40 wa wanamgambo wa Dola ya Kiislamu (IS) kulipiza kisasi kwa wapiganaji hao wa jihadi kuikalia kwa miaka mitatu ardhi ya Iraq wakati wa mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kuuawa kikatili.

Wanawake hao ambao ni wa kigeni walikiri mahakamani kwamba na wao ni waathirika wa IS, walipewa dakika 10 kila mmoja kutetea uhai wao kabla ya majaji kufikia uamuzi wapewe adhabu kali.

Wanawake hao walishutumiwa na mahakama ya Iraq na raia wa kawaida kwa kuwapa msaada waume zao wapiganaji waliosababisha maafa katika eneo walilokuwa wanakalia kuanzia mwaka 2014 hadi 2017.

Utetezi wa wanawake
Mwanamke mmoja mwenye uraia wa Ufaransa aitwaye Djamila Boutoutao, 29, alidai kuwa alidhani alikuwa anaolewa na mwanamuziki wa miondoko ya rap.

“Ni baada ya kuwasili Uturuki kwa ajili ya ‘mapumziko’ ya wiki moja ndipo nilipogundua ya kuwa mume wangu ni mpiganaji wa kijihadi,” alisema Djamila.

“Mimi ni mwathirika. Mume wangu alinipiga na kunifungia kwenye pango na watoto wangu nilipokataa kumfuata (hadi Iraq).’

Djamila ni mmoja wa raia wa Ufaransa wapatao 1,900 na wasafiri wa kigeni wanaokadiriwa kuwa 40,000 waliosafiri hadi Syria na Iraq kujiunga na miliki ya khalifa.

Uchunguzi wa gazeti
Katika hukumu yake ya hivi karibuni, ambako aliomba asitenganishwe na binti yake, Djamila aliwaambia waandishi wa habari wa gazeti la The Guardian: “Nachanganyikiwa hapa.


Nakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha jela maisha. Hakuna anayeniambia chochote, si balozi wetu wala watu ndani ya gereza.”

“Jamani nawasihi msiwaache waondoke na binti yangu. Niko tayari kuwapa fedha endapo mtawasiliana na wazazi wangu. Tafadhali niokoeni.” Takriban wanawake 40 ndio wamehukumiwa kifo na watu wengine 300 wenye mafungamano na IS wameshauawa.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: