MAPACHA WENYE UMRI WA MIAKA 41 WALIOUNGANA NYONGA NA UKE WATAMANI KUSHIKA UJAUZITO TENA
Wakati wengi tumeguswa na mapacha waliofariki huko Iringa Tanzania (soma maajabu yao hapa -maajabu-ya-mapacha-walioungana, Geofrey Chambua anaeleza.
Leo anawaletea kisa cha hawa mapacha walio hai huko nchini India wao wamepewa jina la Spider kutokana na kuungana maungo yao ya nyonga.
Wanaitwa Ayara na Jayara Ratun wana umri wa miaka 41 wamezaliwa Barsirat, Bengala nchini India wana mume mmoja tu kwa muda wa miaka 22 sasa kwa kuwa wana uke mmoja tu, miguu mitatu na mikono ndio inawasaidia kutembea.
Mume aitwaye Gadadhar alipoulizwa anampenda nani kwa dhati alijibu tu kwamba anawapenda wote!.
(Gadadhar replies, “I love either.)
Madaktari wameshawahi kusema ya kuwa wanaweza kuwafanyia upasuaji ili kuwatenganisha lakini wenyewe wamegoma na kusema wanapendelea kuendelea kuwa hivi.
Walishawahi kupata ujauzito na kujifungua ila mtoto wao mwaka 1993 ilikuwa bahati mbaya kwa kuwa alipata wakati mgumu wa kuzaliwa na hivyo mtoto huyu alifariki dunia saa chache baaada ya kuzaliwa.
Mapacha hawa bado wana kiu na ndoto ya kupata mtoto mwingine. Hata hivyo Watabibu wametahadharisha hatari ya wao kubeba ujauzito (sio mimba) kutokana na maumbile yao.
Mapacha hawa yasemekana hutifuana mara kwa mara na licha ya kila mmoja kuruhusiwa kupiga KURA kwa mgombea ampendaye, ombi lao la kufungua amana ya pamoja lilikataliwa ...........Ganga hupendelea sana Samaki ilihali Jamuna yeye mlo wake mkubwa ni kitoweo cha nyama.
Ganga hupenda sana filamu na Muziki (Amitabh) ilihali Jamuna hupenda sana Kulala...wawili hawa wamekataa katu kutengenishwa wakiamini kuumbwa kwao ni mapenzi ya Subḥān Allāh na katu hawawezi kumkana
0 comments:
Post a Comment