BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WEMA SEPETU AFANYIWA UPASUAJI WA KITABIBU MWILINI


Dar es Salaam. Mwigizaji Wema Sepetu, amerejea kutoka nchini India ambapo alienda kwa matibabu.

Meneja wa mlimbwende huyo ambaye amewahi kutwaa taji la Miss Tanzania 2006, Martin Kadinda amesema amerejea juzi, baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo.

“Wema amerejea lakini kwa sasa hawezi kuzungumza kwenye simu anahitaji kupumzika, amefanyiwa upasuaji mdogo na anaendelea vizuri,” amesema Kadinda.

Alipoulizwa kuhusu upasuaji huo, hakuwa tayari kuzungumzia kwa kina badala yake alijibu ni mambo ya wanawake.

“ Ninachoweza kukwamba ni kwamba ni upasuaji mdogo, ndiyo maana alikwenda pekee yake, tena natumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki wake kuwa Wema anaendelea vizuri kiafya,” amesema Kadinda.

Habari kuhusu matibabu ya Wema anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya, zilibainishwa wiki iliyopita baada ya kushindwa kufika mahakamani Mei 29 ili kuendelea kusikiliza kesi yake.

Mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariamu Sepetu alifika mahakamani hapo na kuijulisha kuwa mwanaye anaumwa yupo India kwa ajili ya matibabu. 


Mama huyo alilazimika kuwasilisha nyaraka za kusafiria na kuzionyesha kwenye Mahakama hiyo badala ya za matibabu.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: