BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFADHILI WA ELIMU VIJIJINI HAWA.

Wafadhili kutoka Idara ya Fedha nchini Filand kutoka kushoto Minna Hares, Anthi Turable katikati na Merja Luostainen wakiwa wamejifunika mwamvuli iliyotokana na kunyesha kwa mvua wakati walipotembelea kukagua miradi inayofanywa na Youth Settlement na Aetsa ya ukarabati wa majengo ya madarasa na ofisi za walimu katika shule ya msingi Peko Misegese wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro ambao ulianza mwaka 2006 na kukamilika 2009 kwa ghalama ya zaidi ya sh 50 Mil.

JUMLA ya 98 Mil zimetumika katika miradi mbalimbali ya elimu katika shule za msingi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kwa kukarabati majengo ya madarasa, nyumba za walimu na kuandaa vitabu vya elimu kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na pili katika shule kumi za wilayani hapo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika kijiji cha Peko Misegese katika wilaya ya Mvomero mkoa hapa Mratibu wa Miradi wa shirika lisilo la kiserikali la Elimu na Mazingira, Sarafina Ritter alisema jumla ya kiasi hicho kimetumika katika miradi mitatu ya ukarabati wa majengo ya madarasa ya shule za msingi, ujenzi wa nyumba mpya za walimu na kutengeneza vitabu vya kutoa elimu ya afya kwa shule kumi za msingi katika wilaya hiyo.

Alizitaja shule zilizonufaika na mradi huo kuwa nipamoja na Ijara,Ndole,Peko Misegese, Pinde, Mogoigwa, Kibindu, Vinile, Kibati, KwaKonje na Yowe ambapo vitabu vingine vitaghalimu kiasi cha shilingi 15 Mil kwa wanafunzi wa madarasa la tatu na nne kuwa viko katika hatua za mwisho kumamilika huku madarasa ya tano, sita na saba vikiwa katika hatua za awali ya maandalizi yake.

Ritter alisema wakati wa ugeni wa wafadhili kutoka idara ya fedha ya nchini Filand walipotembelea kukagua miradi hiyo katika kijiji hicho ambapo alitaja mradi wa kwanza kuwa ni ukarabati wa shule ya msingi Peko Misegese iliyopo katika kata ya Mlali ambao ulianza mwaka 2006 na kukamilika mwaka 2009 ambapo ulighalimu kiasi cha zaidi ya sh 50 Mil ikiwemo na kuwapatia wanafunzi wa shule hiyo madawati 20 hali ambayo ilitokana na wanafunzi 60 kukaa katika mawe wakati wa masomo yao huku ikiwa na jumla ya wanafunzi wanafunzi 525.

Aidha aliitaja miradi hiyo ambayo imetekelezwa kwa ushirikiano wa asasi za kiraia za Youth Settlement na Aetsa ambapo mradi huo umeinufaisha shule hiyo imenufaika kwa ukarabati wa madarasa matano na ofisi za walimu ambapo awali madarasa hayo yalikuwa machakavu na shule ya msingi Pinde ilifaidika kwa ukarabati wa majengo matatu ya madarasa , ofisi moja ya walimu na ujenzi wa nyumba mpya moja ambapo inatumiwa kwa familia mbili kwa dhamani ya 30 Mil.

Ritter alisema shilingi 18 mil zingine zimetumika katika mradi wa majaribio wa kutengeneza vitabu 2000 kwa wanafunzi wa madarasa ya kwanza na darasa la pili kwa shule kumi ambapo wamegawiwa vitavu 2000 vya kutoa elimu ya afya kwa kila mwanafunzi ikiwa mwanafunzi hupatiwa kitabu kimoja.

Mratibu huyo ametoa wito kwa mashirika mengine kuelekeza nguvu kwa kutoa misaada katika shule za vijijini kutokana na utafiti uliofanywa na shirika hilo limebaini miradi mingi kufanyika maeneo ya mijini na wanafunzi wanaosoma shule za vijijini kuwa wanamahitaji mengi.




Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: