TIMU ya soka ya Wizara ya Mambo ya Ndani imetoa onyo katika ufunguzi wa mashindano ya Mei Mosi Cup baada ya kuikandamiza Tumbaku Fc katika mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro kwa bao 7-2.
Wakicheza kwa kutandaza soka safi na kasi chini ya mwalimu mkuu wa timu ya wizara ya Mambo ya Ndani, Jonas Mahanga, ilianza kuhesabu kalamu ya mabao kupitia kwa mshambulijia wao tegemeo Nicolaus Marco aliyefumania nyavu za wapinzani wao kwa kufunga bao bao tatu kwenye dakika ya pili, dakika ya 38 na dakika 47.
Katika mchezo huo timu ya Tumbaku Fc inayonolewa na Mwalimu mkuu, Boniface Njohole ilijaribu kujitutumua na kupata bao la kwanza lililofungwa na Andende Amandi katika dakika ya 43 kwa njia ya penalti baada ya mlinzi wa wizara ya Mambo ya Ndani Salimin Mohamed kufanya madhambi eneo la hatari na mwamuzi, Mohamedi Thoufil, kuamuru ipigwa penalti hiyo kabla ya Salehe Mohamedi kufunga la pili katika dakika ya 68.
Mabao mengine ya wizara ya Mambo ya Ndani yalifungwa na Imani Steven aliyefunga bao mbili katika dakika ya 55 na lingine katika dakika ya 89 huku Ally Shabaani akichangia kwa kutandika bao la tano kwa kufunga bao mbili kwenye dakika 76 na 90 na kuhitimisha ushindi huo mnono wa bao 7-2.
Michuano hiyo inaendalea tena kwa kuzikutanisha timu za Alliance One na timu ya Ukaguzi utaochezawa uwanja wa Jamhuri ambapo mashindano hayo yanashirikisha timu kumi zikiwemo za wizara na Idara za serikali, Ofisi ya Mkuu wa mkoa (RAS) Makampuni ya Umma na Makampuni binafsi ambapo katika mchezo wa fainali unatarajiwa kuchezwa Aprili 29 na washindi kukabidhiwa zawadi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi katika uwanja wa Jamhuri.
0 comments:
Post a Comment