BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AJALI YA BASI LA ABOOD MWIDU PWANI.

BASI la kampuni ya Abood Bus Service la mkoani Morogoro T 969 ALY limeacha njia na kupinduka katika eneo la Mwidu katika barabara kuu Dar es Salaam-Morogoro mkoa wa Pwani na kujeruhi watu 45.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mwidu mkoani Pwani baada ya Lori lenye namba ya usajili T 892 AFL wakati likijaribu kulipita basi la Upendo T 482 ANA katika eneo hilo
ambapo dereva wa basi la Abood Hussein Mohamedi (39) alijaribu kuinusuru ajali hiyo kwa kukwepa kugongana uso kwa uso kabla ya kuacha njia na kupinduka.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani eneo la Tukio Absaloum Mwakyoma alisema ajali hiyo imetokea baada ya lori lenye namba ya usajili T 892 AFL wakati likijaribu kulipita basi la Upendo T 482 ANA katika eneo la Mwidu mkoani humo ambapo dereva wa basi la Abood Hussein Mohamedi (39) mkazi wa Morogoro wakati katika jitihada za kuinusuru ajali hiyo isitokee alijaribu kulikwepa Lori hilo kwa kugongana uso kwa uso kabla ya kuacha njia na kupinduka.

Lile lori lilikuwa likiovertake basi la Upendo T482 ANA katika mlima wa kijiji cha Mwidu lakini kabla ya kuovertake huyu dereva wa Upendo alimzuia dereva wa Lori asiovertake kwani mbele kulikuwa na basi linakuja ambalo ni Abood lakini hakufuata utaratibu huo ndio ajali hiyo ilivyokea, alisema Kamanda Mwakyoma.

Kamanda Mwakyoma alisema jumla ya majeruhi 45 walijeruhi katika ajali hiyo na kukimbizwa katika Hospitali ya jirani ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata huduma na ikijuisha wanaume 22 na wanawake 23.

Wakati huo huo Afisa Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro Obadia Peter alisema kuwa katika ajali hiyo walipokea majeruhi 45 na kati ya hao wanawake 23 na wanaume 22 na kati yao 37 walitibiwa na kuruhusiwa na majeruhi nane walilazwa kwenye hospitali hiyo.

Aliwataja majeruhi waliolazwa kuwa ni Omari Mfaume (16) mkazi wa Kinole Morogoro Vijiji, Amina Hamed (35) mkazi wa Manzese mjini Morogoro, Rehema Ally mkazi wa Msamvu Manispaa ya Morogoro,Saraha Mwenga (25) na Awas Saidi (24) mkazi wa Manzese Manispaa ya Morogoro.

Aliwataja majeruhi wengine kuwa ni mtoto Nija Shaibu mmoja na nusu, Rehema Selemani (20) mkazi wa Mikese Morogoro Vijijini na Chrisitina Migunga (22) mkazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro.

Muuguzi huyo alisema majeruhu, Omari Mfaume (16) atasafirishwa kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili baada ya kuumia mguu wa kulia huku wengine wakisubiria uchunguzi zaidi wa daktari.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: