KAMATI ya uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Morogoro (MRFA) wameiandikia chama cha soka mkoa huo kufuta uchaguzi wa kujaza nafasi zilizopo wazi za Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji baada ya wagombea kususia kuchukua fomu hizo mjini hapa.
Akizungumza na gazeti hili Kaimu Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi Chama soka mkoa wa Morogoro (MRFA) Roman Luoga, mjini hapa alisema wagombea wamesusia kuchukua fomu za kujaza nafasi zilizopo wazi za Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji mpaka sasa kutokana na kutochukua fomu hizo na kuwa hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu hizo mpaka sasa ambapo kamati hiyo kulazimika kufuta uchaguzi baada ya kuisha kwa muda wa kuchukua fomu ambapo ilikuwa mei 1 hadi mei 7.
Muda wa kuchukua fomu ilikuwa mei 1 hadi 7 lakini kutokana na wagombea kutochukua fomu hivyo hakuna uchaguzi na kamati yao imelazimika kuandikia barua TFF Mkoa kuitarifu kuwa mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu na muda wake umeisha hivyo TFF Mkoa tumewaachia jukumu la kupanga upya kalenda nyingine ya kuanda uchaguzi wa kujaza nafasi hizo. Alisema Luoga.
Kaimu Katibu Mkuu huyo alitaja kiasi cha kuchukua fomu kuwa ni shilingi 100,000 kwa kila nafasi moja na kutaja sifa za wagombea kuwa ni lazima awe raia wa Tanzania, elimu ya sekondari na asiwe na hati ya makaosa ya jinai pamoja na awe na uzoefu wa miaka mitatu katika soka.
Wakati huo mmoja wa wadau wa soka katika Manispaa ya Morogoro, Samuel Msuya, ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo alisema hali ya wagombea kususia kuchukua fomu za kugombea nafasi za hizo inatokana na wagombea kupiga mahesabu ya kukaa madarakani kwa muda wa miezi sita hivyo na kuwa ghalama itakayotumika katika kampeni na ile ya fomu ya sh 100,000 itakuwa kubwa na kukaa kwa mfupi hivyo wameona kusubiri mpaka uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani mwezi wa nane kutokana na kalenda ya TFF mkoa.
“hawa wagombea wameona mbali kwa kupiga mahesabu kwani ukiangalia kiundani wakataa kwa muda wa miezi sita hivyo wameona bora wasubiri uchaguzi mkuu ujao ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwakani” alisema Msuya.
0 comments:
Post a Comment