BAO LA KALE.
Wahenga walinena ya kuwa “ya kale ni dhahabu” Msemo huo umedhihirisha katika safu ya milima ya Uluguru mkoa wa Morogoro baada ya kugundulika kuwepo kwa utajiri mwingi wa mambo ya kale ambayo ni vivutio vya utalii wa ndani.
Ni mwendo wa saa kumi kwa usafiri wa basi kufika katika kitongoji cha Kibakana kabla ya kubadilishwa jina na kuita Usolo, jina ambalo limepata umaarufu mkubwa katika kata ya Lunda Morogoro Vijijini.
Umaarufu wa kitongoji cha Usolo umetokana na tukio la kihistoria la karacha wawili, mtu na mpwa wake Kingalu wa kwanza, Mleke Mwanamsumi Mwana Kulinyangwa na mpwa aliyefahamika kwa jina moja la Hega.
Kitongoji cha Usolo ni maafuru wilayani humo kutokana na tukio la kihistoria la karacha wawili wa mila na desturi, Chifu Kingalu wa kwanza na mwenzake Chifu Hega kutunishiana misuli ya kutumia ncha ya visigino vyao kuchimba vishimo vua usolo juu ya mwamba wa jiwe.
Inasadikiwa kuwa wahenga hao walikuwa wakigombania madaraka kiutawala katika safu ya milima ya Uluguru karne ya tatu zilizopita.
Kitongoji cha Usolo kipo katika makutano ya mito miwili ya Mngazi na Mtombozi, ambapo asili ya kuwepo jina hilo ni kutokana na tukio la kuwepo kwa mashimo ya usolo yanayosadikiwa kuchimbwa na wahenga hao (Kingalu wa kwanza na Hega) alama hizo zinapatikana hadi sasa.
Mkoa wa Morogoro wenye wakazi zaidi laki nne kwa kadri ya sensa ya mwaka 2002 inasadikiwa kuwa na vivutio vingi ambavyo vinaweza (kutumika) kuandaliwa mazingira mazuri ya wananchi kutembelea maeneo hayo kama kuenzi utalii wa ndani.
Safu ya milima ya uluguru inayopatikana katika mkoa wa Morogoro ina bainuai za kipekee ambazo hazipatikani maeneo mengine duniani zaidi ya safu ya milima ya uluguru.
Kwa mujibu wa shirika la kuhifadhi na kulinda bainuai (WCST) katika milima ya uluguru liliwahi kufanya utafiti na kubaini bainuai hizo kuwa ni mbega, kinyonga, ndege aina ya kurumbizi na wengine wengi kadhaa wa kadhaa zilizopo katika safu ya milima hiyo.
Mbali na kuwepo kwa vivutio hivyo pia kuwa mwamba unaotoa chemchem ya maji ya moto ambayo huweza kuivisha yai kwa dakika tano na mtu akaweza kula papo hapo.
Safu hiyo hiyo ya milima ya uluguru ina utajiri wa mambo mbalimbali yanayoweza kutembelewa na kuipatia serikali fedha au kipato kwa wale wataofanya utalii wa ndani iwapo taratibu nzuri za kiusalama kwa watalii zikiandaliwa.
Lakini zipo changamoto mbalimbali zilizopo kwa upande wa serikali hususani idara za utamaduni kuendeleza maneo ya kihistoria kama safu ya milima ya uluguru na mengine yanayofanana na hayo.
Inasadikiwa katika ushindani huo Chifu Kingalu alishinda kwa kuchimba visigino vya matundu 30 huku kwa upande wa Chifu Hega aliambulia visigino 16 pekee.
Kutokana na matokeo hayo wanamapokeo wa historia wameelezea kuwa upande wa Kingalu aliweka mipaka kuwa kutoka eneo la hilo la mto Mtombozi kuelekea Kisaki lilimilikiwa na Hega, huku eneo la upande wa mwingine wa kuelekea Kinole kuwa ni himaya ya Kingalu, ambapo ndiko kwenye makazi ya Chifu Kingalu Mwanabanzi wa (14) mtawala wa jadi kwa kabila la waluguru hadi hivi leo.
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Filauni, mwandishi wa makala hii ni miongoni mwa watu waliofika katika kitongoji hicho na kushuhudia uwepo wa alama hizo na ambazo kwa lugha ya kiluguru ni “kisegeyu” ikimaanisha unyayo wa binadamu.
Kwa mujibu wa Hamisi Mbena ametaja miamba mingine ya ajabu iliyopo katika safu ya milima ya uluguru kwenye majabali yalipo milimani na kando kando yam to Mtombozi kuna miamba miwili yenye utupu na upande wa pili.
Ni vishimo hivyo vya usolovilikutwa katika mwamba wa jabali lililopo kando kando ya mto Mtombozi huku kukiwepo vinyesi vya wanyama wa mwituni.
Mwandishi alipotaka kusafisha vinyesi vivyo alizuiliwa na mwenyeji kwa kile kilichodaiwa kuwa eneo hilo halisafishwi toka vichimbwe na wahusika.
“yeyote atakaye jaribu kusafisha vishimo hivi atapoteza maisha ” Alimtahadharisha mwandishi aliyefika katika eneo hilo Mbena.
Aidha, mto Mtombozi una kawaida ya kujaa maji na kupelekea kufurika mwamba wenye usolo huo ambao iwapo mamlaka husika wataliendeleza kwa kuwekeza eneo hilo kungekuwa ni eneo zuri la kufanya utalii wa ndani hususani kuenzi mila na desturi za kiafrika.
Kwa mujibu wa dodoso zilizopatikana katika eneo hilo la ushindani uliojitokeza kati ya Chifu Hega na Chifu Kingalu ni kushimba vishimo vinavyoringana na kanuni ya mchezowa solo(bao) kuwa na vishimo 36 kwa muda mfupi.
Hii inatokana na jiographia ya eneo hilo kuwa na miunuko mingi kwa msafiri anayependa kutembelea eneo hilo hana budi kumtafuta mwenyeji wa kumpeleka eneo hilo.
Ili kufika katika eneo hilo njia inayotumika ni zile za mashambani ni kuna njia za uchochoroni huku kukiwa na maporomoko makali sana yanayoweza kuhatarisha afya ya mtu.
“Njia hii tunayopita ina maporomoko makali unahitajika uvumilivu kwani kuna miamba mingi unayoiona ni makazi ya chatu wa milimani ” alihadhalisha Hamisi Saidi Mbena (30) aliyeambatana na mwandishi wa habari kuelekea kitongoji cha Usolo.
Mbena ambaye alikuwa ni mwongozaji njia kuelekea eneo la usolo maafuru kwa jina la Kisegeyu maana yake ‘unyayo’ kwa kabila la waluguru.
Dhana ya kisegeyu inatokana na ncha ya kisigino kilichotengeneza usolo katika mwamba kati ya viongozi wa (jadi) mila Kingalu kwa upande mmoja na Hega kwa upande wa pili vishimo hivyo vya usolo vilikutwa katika mwamba wa au jabali lililopo kandokando ya mto Mtombozi huku kukiwepo vinyesi vya wanyama mwitu.
Mwandishi alipotaka kusafisha eneo hilo alizuiwa na wenyeji kwa kile kilichodaiwa kuwa eneo hilo halisafishwi na binadamu toka tukio hilo lilipotokea.
Mzee John Henry (73) alieleza juu ya asili ya usolo huo kuwa kulikuwa na ushindani na tambo za nguvu za kiutawala baina ya viongozi wa mila, kiongozi wa kabila la waluguru Chifu Kingalu na chifu Hega.
Ushindani huo ulionyeshana umwamba na uwezo wa zaida aliyepewa kila mmoja.
Inasadikiwa kuwa watawala hao walikuwa na vita vya maneno lakini ilienda mbali zaidi kwa kuonyesha nguvu walizonazo kwa vitendo.
Walikubaliana kwenda kuweka mipaka ya utawala wao katika makutano ya mto Mtombozi na mto Mngazi iliyoungana na kutengeneza mto mmoja wa Mvuha.
Aidha, taarifa zilizopatikana kwa baadhi ya wanajamii waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi zinaelezwa kuwa miamba hiyo miwili walionyeshana mbwembwe kwa kuchimba mashimo ya usolo kwa kutumia ncha ya visigino vyao katika miamba ya mawe iliyopo katika mto Mtombozi.
Eneo la usolo ambalo linaweza kuitwa mwamba wa historia lipo umbali wa kilometa saba kutoka barabara kuu iendayo Kisaki ambako gari au pikipiki inayoweza kufika achilia mbali baiskeli.
Hatua iliyochukuliwa kwa mujibu wa wazee John Henry ni kulishwa kitu kinachosakiwa kuwana nguvu ya kubaini mkorofi nani kati koo hizo.
“Toka wakati huo eneo hilo la miti mitatu lilitumika kufanya tambiko hususani wakati wa mavuno ili …………..na kufanya eneo hilo kuwa ni kumbukumbu ya mapigano ya koo hizo mbili .”
“Miti hiyo mitatu ilikuwa na kukomaa lakini kutokana na tama baadhi ya watu wachache walikuja kuikata na kuichana mbao” alisema Mzee John na kuongeza,
“Kumbukumbu toka miti hiyo ilipokutwa na kuchanwa mbao litoweka hakuna tena utaratibu wa kupeleka mazao wakati wa mavuno”.
Kituko kingine ni kuwepo kwa miamba yam awe inayosadikiwa kutengenezwa usolo kwa kutumia ncha ya kisigino cha binadamu.
Miamba hiyo ipo makutano ya mto Mtombozi na mto Mngazi ambapo kutokana na kuwepo kwa tukio hilo eneo hilo lilipewa hadhi kwa kupewa jina la Kitongoji cha Usolo.
Aidha baadhi ya wananchi wanaishi kuzunguka safu ya milima ya uluguru wamebainisha baadhi ya vivutio hivyopo katika maeneo yao ni pamoja na miamba ya asili yenye umbo midhiri ya matiti ya mwanamke inayopatikana katika eneo la Matombo Morogoro Vijijini.
Matombo kwa tafsiri ya lugha ya kabila ya waluguru ni matiti ya mwanamkehivyo kutokana na kuwepo kwa miamba hiyo wenyeji waishio katika eneo hilo wamelipa hadhi eneo hilo.
“Ndugu mwandishi eneo la Matombo asili yake ni miamba miwili mithiri ya matiti ndio chimbuko la mji wa Matombo” alisema Mzee John mkazi wa kitongoji cha Tambiko.
Akieleza zaidi Mzee John ambaye alielezea historia ya kitongiji cha Tambiko kwamba lilitokana na mapigano ya koo mbili zilizogombea ardhi, Wachuma katika eneo la hilo la mapigano kulikuwa na miti mitatu ambapo ugomvi huo ulipelekea aitwa mganga aliyeaminiwa kuwa na uwezo wa kutoa dawa ya kubaini kiini cha matatizo na kutoa adhabu kwa mkosaji.
0 comments:
Post a Comment