NA MDAU WA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI, SOSTHENES NYONI.
KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic Januari 25 mwaka huu alitangaza rasmi kukatiza mkataba wake wa kuifundisha klabu hiyo kwa kukabidhi barua kwa uongozi akiwa amebakiza miezi kabla ya kumalizika mkataba wake Aprili mwaka huu.
Hatua ya Papic kutangaza kujiondoa rasmi kuinoa Yanga inafuatia wiki kadhaa za marumbano kati yake na uongozi wa klabu hiyo hasa baada ya viongozi wao kutangaza kumwajiri aliyekuwa kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Fredy Felix Minziro.
Awali kabla ya Papic kuiambia Mwananchi juu ya uamuzi wake huo kulikuwa na kikao baina yake na uongozi wa Yanga uliofanyika jana kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana.
Mapema kabla ya kufikia uamuzi huo Papic aliliambia gazeti dada ya Mwananchi, Mwanaspoti muda mchache kabla kuikabili Polisi Dodoma katika mechi ya ligi kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kumwajiri Minziro kuwa msaidizi wake bila ridhaa yake ni dharau kubwa hivyo hataweza tena kuifundisha timu hiyo.
Akizungumza na Mwananchi baada ya kumalizika kikao kati yake na uongozi wa Yanga, Papic alisema,"Kama nilivyosema awali kuwa nitaondoka hivyo natangaza rasmi mkataba wangu na Yanga umekwisha.
"Sitaweza kuongea mengi zaidi muda huu kwani nimechoka isipokuwa jambo la msingi na ambalo ninaweza kueleweka ni kwamba nimejiuzuru.
"Kuna vitu vichache tu vya kumalizana nao pamoja na kushughulikia tiketi na Jumatatu nitaondoka kurudi Serbia,"alisema Papic.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment