MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro Amiri Juma Nondo ametoa amri ya kuwatimua wafanyabiashara wa matunda endapo wataendelea kutotimiza masharti ya usafi baada ya kumaliza kazi ya kuuza matunda maeneo ya katikati ya Manispaa hiyo kwa kurundika uchafu kwenye mapipa ya taka ngumu kipita kiasi na kusababisha kero kwa watumiaji wengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya mji huo Meya huyo Amiri Nondo alisema hayo wakati alipokuwa akiangalia hali ya usafi katika stendi hiyo na mitaa mbalimbali ya mji huo ambapo alibaini lundo la taka zikiwa zimeelemea mapipa ya kuhifadhia uchafu kutokana na wafanyabiashara kutupa uchafu huo kwenye mapipa yaliyopo katika mji huo.
Meya huyo aliwataka wafanyabiashara hao kuacha tabia ya kujaza uchafu kupita kiasi kwenye mapipa hayo na badala yake wapunguze uchafu huo kabla ya kuja nao mjini ambapo uchafu huo huletwa na wafanyabishara kwa lengo la kuhifadhia matunda yao ili yasiharibike wakati wa kuyabeba kutoka kwa wakulima ambapo alitoa onyo la kutoendelea na tabia hiyo na kufanya hivyo kutawafanya mgambo wa Manispaa hiyo kuwatimua katika maeneo hayo kwani wapo kinyume naa taratibu za kisheria.
"hawa wafanyabiashara wanafanya biashara kinyume na taratibu za Halmashauri ambazo zinamtaka kila mfanyabiashara akauzie biahsra yake sokoni na sio katikati ya mji jambo hilo halipo kabisa lakini wanataka kujiharibia wenyewe wangetumia ustarabu wao kwa kufanya usafi sehemu wanaouzia matunda kuondoka nao uchafu isingekuwa tatizo kwani kufanya biashara nyati za jioni na usiku husaidia wafanyakazi ambao wamekosa muda wa kwenda sokoni na kupata huduma hiyo ya kununua matunda kwao lakini wao hulundika uchafu kupita kiasi katika mapipa na wengine huuacha uchafu huo sehemu hiyi hiyo wanazouzia si jambo la kiungwana". alisema Nondo.
Nondo alisema kuwa tabia hiyo imekuwa ikimkera kutokana na uchafu huo ambapo aliahidi kuonana na mkuu wa kitengo cha afya katika Manispaa hiyo ili kuangalia namna ya kuweka utaratibu mzuri wa wafanyabiashara hao wasiendelee na tabia hiyo kueneza uchafu kwenye mapipa hayo.
“lengo la kuweka mapipa yale sehemu mbalimbali za mitaa ya mji wetu ilikuwa ni kwa ajili ya wapiti njia kutupa taka ndogo ndogo kwenye mapipa hayo lakini hili la wafanyabiashara wa matunda kurundika uchafu wao na kujaza katika mapipa limekuwa tatizo jipya lakini tutalitafutia ufumbuzi kwani kuachwa kwao kufanya biashara nyati za jioni isiwe sababu ya kutuharibia utaratibu wetu hatutaweza kuvumilia kazi hiyo ikiendelea”. alisema Nondo.
Aidha Nondo aliwataja baadhi ya vinara wa kueneza uchafu baada ya shughuli zao za kuuza matunda katikati ya mji huo kwenye mapipa kuwa ni wafanyabiashara wa kuuza ndizi, mananasi na maembe ambao wamekuwa na tabia ya kulundika taka hizo baada ya kuhifadhia bidhaa zao kwenye mapipa ikiwa ni baada ya kumaliza kazi yao ya kuuza matunda yao wakati wa usiku wa kuondoka maeneo hayo.
Akizungumzia suala la kutapakaa kwa taka ngumu kando kando ya mapipa makubwa ya kuhifadhia taka katika maeneo mbalimbali ya mji huo ambako kunakosababishwa na uchafu kuwa mwingi Nondo alisema tatizo hilo kweli lilijitokeza hivi karibuni kwa sababu ya magari ya kuzoa taka ngumu yalikuwa mabavu jambo ambalo ilisababisha kwa hali hiyo lakini magari hayo kwa sasa yamefanyiwa matengenezo na yanaendelea na shughuli ya uzoaji taka ngumu mchana na usiku ili kuondoka taka maeneo yote ya mji huo.
Nondo alisema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa na mikakati kabambe ya kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya usafi ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yanayozunguka Manispaa na kuleta taswira nzuri ya mji huo ambao umekuwa kioo kwa mikoa ya jirani.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MEYA KUWATIMUA WAFANYABIASHARA WA MATUNDA ENDAPO HAWATAFUATA TARATIBU ZA USAFI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment