BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WADAU WA SOKA MORO WATISHIA KWENDA MAHAKAMANI ENDAPO TFF HAWAWEKA UTARATIBU WA KUKAGUA UPYA VYETI HALISI VYA WAGOMBEA.

WADAU wa soka mkoani Morogoro wanaliomba shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuingilia kati suala la uchaguzi mkuu wa chama cha mpira wa miguu Morogoro (MRFA) kwa madai ya baadhi ya waombaji kutotimiza sifa za kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika Januari 15 mjini hapa.

Sifa hizo ni pamoja na kupata viongozi bora na waadilifu wanaotokana na sifa zinahitajika kwa mujibu wa katiba ya chama cha mpira wa miguu mkoani hapa (MRFA) ambayo kupitia ibara ya 29 ukurasa wa 18 kifungu cha 1 mpaka 7 katika ukurasa wa 19 zimeelezwa sifa za wagombea.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa Leonard Massawe na Ferinus Mrope walisema kuwa sifa za baadhi ya wagombea hazikidhi kugombea nafasi za uongozi katika chama cha mpira wa miguu (MRFA) ikiwemo pamoja na kutokuwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na kudaiwa kuwa baadhi yao wakiwa na vyeti vya darasa la saba.

Kwa mujibu wa katiba ya MRFA ibara ya 29 sifa za wagombea kifungu cha pili ukurasa wa 18 katika katiba hiyo inamtaka mgombea kuwa na sifa za kiwango cha elimu ya sekondari kuanzia kidato cha nne na kuendelea.

Nafasi ambazo zinatiliwa mashaka na wadau katika uchaguzi huo kwa waombaji hao ni pamoja na mgombea nafasi ya mwenyekiti, katibu mkuu, mwakilishi wa vilabu pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji, walisema wadau hao.

Katika nafasi ya mgombea wa mwenyekiti anadaiwa kutowasilisha cheti halisi katika mkutano wa usahili ambao ulifanyika januari mosi mwaka huu katika ukumbi wa Masuka Village mjini hapa akiwemo pamoja na mgombea wa nafasi ya katibu mkuu na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ambao katika usahili huo baadhi ya wagombea hawakuweza kuwasilisha vivuli vya vyeti vyao na kudai kutokana na hilo wameingiwa na mashaka juu ya waombaji hao katika kuongoza michezo katika chama cha mpira wa miguu (MRFA).

Aidha wadau hao walisema kuwa katika nafasi ya mgombea wa mwakilishi wa vilabu kutoka wilaya ya Mahenge anadaiwa kuwa sio mwakilishi halali wa wilaya hiyo licha ya katibu mkuu wa chama cha wilaya kusita kuthibitisha kutambuzi wa mwakilishi huyo wakati akiongea kwa njia ya simu ambapo alidai kuwa taarifa zisizo rasmi alidai anawania nafasi hiyo kutoka klabu ya vijana wilayani humo.

Pia wadau hao walisema kuwa katika nafasi ya kugombea wagombea wa kamati ya utendaji wa MRFA wanadai baadhi yao hawana vyeti vya kidato cha nne huku wengine wakidaiwa kuwa na vyeti vya darasa la saba.

Wadau hao wametoa ushauri kwa katibu mkuu mpya wa TFF kuweka utaratibu wa kukagua upya vyeti halisi vya wagombea chini ya wataalam kutoka baraza la mitihani nchini (NEKTA) siku tatu kabla ya uchaguzi na endapo shirikisho hilo hatazingatia ushauri huo wa wadau wa soka mkoani Morogoro watakwenda kuweka pingamizi uchugazi huo kwenye vyombo vya sheria kuzuia uchaguzi huo mpaka taratibu zitakapofuatwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: