MKUU wa wilaya ya Morogoro Said Mwambungu amewataka wazazi kuchukua hatua thabiti kwa watoto wao wanapoanza tabia ya udokozi wakiwa wadogo, na kwamba tabia hiyo ikiachwa ndiyo mwanzo kikuu cha kuzalisha kundi la uharifu hapa nchini.
Akizungumza katika na wahitimu wa mafunzo ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa vijana 80 wa kata ta Tungi katika Manispaa ya Morogoro walioshiriki mafunzo hayo alisema tabia hiyo ikiachwa bila ya kukemewa na wazazi au walezi ndiyo kulizalisha kundi la vijana wanajiingiza katika vitendo vya uhalifu na kuleta athali ndani ya jamii.
Mwambungu aliwataka wazazi kuchukua hatua thabiti katika hatua za mwanzo kwa mtoto ambao wanaanza tabia ya udokozi wakiwa mdogo na kwamba anapoachwa bila kuthibitiwa tabia hiyo hukomaa na kuzalisha majambazi.
“ Wazazi mnatakiwa kuwathibiti watoto katika hatua za awali hatua za udokozi ndiyo mwanzo wa kuwa na jambazi mtoto anapoanza kidogo kidogo kudokoa vitu vidogo mwisho wake ni kuwa jambazi”. Alisema Mwambungu.
Alisema kuwa uhalifu unaweza kupungua ama kuisha kabisa ikiwa utachukiwa kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, kata hadi taifa, na kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia kutokomeza kabisa tabia hii mbaya katika jamii ya watu wastarabu.
Aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuwatetea watu kwa mambo maovu na badala yake wawatetee kwa mambo mazuri, na kwamba inapotokea mtu amefanya uhalifu aachwe ili sheria ifuate mkondo wake na kusiwe na tabia ya kuwatetea wahalifu.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha polisi Jamii Mkoa wa Morogoro (ASP) Isack Mushi, alisema kuwa kitengo hicho kimekuwa kikabiliwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi wanaopatiwa mafunzo hayo.
Aliitaja mmoja ya changamoto hizo kuwa ni ufinyu wa nauli kwa wananchi wanaopenda kuhudhuria mafunzo hayo wanaoishio mbali na kituo cha mafunzo.
Aidha alitoa wito kwa wananchi wanaopenda kupewa mafunzo hayo kutoa taarifa kwenye kitengo hicho ili waweze kuendesha mafunzo hayo katika maeneo husika kwa kukusanya watu waliopo maeneo hayo ili kuimarisha ulinzi katika ngazi ya kaya.
Akisoma risala Damson Chilongola ambaye ni mhitimu wa mafunzo hayo aliliomba jeshi la polisi kuendelea kutoa mafunzo hayo sehemu nyingine ambazo mafunzio hayo hayajatolewa ili iwe rahisi kwa kila mwananchi kufahamu jukumu lake la polisi jamii na ulinzi shirikishi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment