BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZAZI WACHANGA SH 4.7MIL KUONDOA KERO YA MADAWATI MORO.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bungo Manispaa ya Morogoro, Roman Luwoga kushoto (mwenye shati nyekundu) akiwa na baadhi ya mwalimu na wanafunzi wa shule hiyo wakisomba madawati yaliyotokana na michango ya wazazi baada ya kutengeneza madawati 70 ikiwa na lengo la kuondokana na tatizo la madawati yakiwa na thamani ya sh 4.7Mil.

KIASI cha sh 4.7Mil kimewezesha kuondoa tatizo la madawati katika shule ya msingi Bungo iliyopo katika kata ya Boma Manispaa ya Morogoro kupitia michango ya wazazi baada ya shule hiyo kununua madawati 70 ikiwa na lengo la kuondokana na kero ya wanafunzi katika shule hiyo kurundikana katika dawati moja na kuwawezesha wanafunzi wawili kutumia dawati mmoja mjini hapa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano shuleni hapo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Msingi Bungo Manispaa ya Morogoro, Roman Luwoga alisema kupitia kamati ya shule hiyo iliadhimia kuwepo kwa mpango wa kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa katika dawati moja wanafunzi watatu hali iliyopelekea ununuzi wa madawati hayo 70 ikiwa na lengo la kuondoa kabisa kero hiyo wakati wa masomo kwa wanafunzi hao.

Luwoga alisema kuwa kupitia kamati ya shule hiyo wazazi waliweza kuchanga kiasi cha sh 4.7Mil kwa ajili ya ununuzi wa madawati hayo pamoja na matumizi mbalimbali ya shule hiyo.

“hizi ni nguvu za wazazi walioamua kuchangia fedha ili kuondoa tatizo la hilo kupitia kamati yao ya shule na kufanya wanafunzi kwa sasaa wanatumia dawati moja wanafunzi wawili badala ya awali ambapo dawati moja lilikuwa linakaliwa na wanafunzi watatu ambapo hali hiyo ilikuwa kero kwa wanafunzi wakati wa masomo yao.” alisema Luwoga.

Aidha Luwoga alisema kuwa kabla ya ununuzi wa madawati hayo 70 hakukuwa na tatizo la wanafunzi katika shule hiyo kukaa chini wakati wa masomo isipokuwa tatizo likukuwa kwa wanafunzi wa madarasa mawili ambayo yalikumbwa na tatizo la dawati moja kukaliwa na wanafunzi watatu lakini kupitia mpango huo shule hiyo imefanikiwa kuondoa tatizo hilo na kuwa na akiba ya madawati ya ziada.

Pia mwalimu mkuu huyo alisema kuwa amekuwa akiwapa ovyo wanafunzi kwa kupita kila darasa kuanzia watoto wa chekechea, darasa la kwanza hadi darasa la saba kuacha tabia ya kucheza juu ya madawati hasa pindi mwalimu anapotoka darasani na badala yake kama watakuwa wamemaliza kazi ya kuandika wafanya kuzipitia kazi za nyuma kwa kujikumbusha kwa kusoma badala ya kufanya vurugu darasani ambapo kutokana na kutoa somo hilo kwa wanafunzi madawati hayo yatadumu kwa muda mrefu.

“unajua wanafunzi ni watundu sana hasa hawa wa shule ya awali, darasa la kwanza hadi darasa la nne yaani mwalimu anapokosekana kwa dakika tatu au tano darasa linakuwa na vurugu tupu kutokana na utoto wao lakini tunajaribu kudhibiti hali hiyo kila siku na wanapofika darasa la tano na saba tabia hiyo huiacha kwani akili yao inakuwa tayari imekomaa katika masomo.” Alisema Luwoga.

Luwoga alisema baada ya yeye kupita kila darasa kutoa somo kwa wanafunzi juu ya utunzaji wa madawati pia kazi hiyo ametoa agizo kwa kila mwalimu wa shule hiyo kuwakemea wanafunzi juu ya kucheza kwa kupanda juu ya madawati kwani kufanya hivyo madawati hayo yatasababisha kuharibika mapema.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: