BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOCHA WA JTK RUVU AIBUKA NA MAJIGAMBO LIGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA NETIBOLI .

KOCHA mkuu wa timu ya mpira wa netiboli ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani, Argentina Daudi ameibuka na kauli ya kufanya vizuri sambamba na kutwaa ubingwa wa mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa katika michuano iliyoanza kutimua vumvi kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri februari 16 mjini Morogoro.

Mashindano hayo ambayo yanatarajia kushirikisha timu kumi na nane (18) na kupandisha timu nne ambazo zitaingia kucheza ligi daraja la kwanza msimu huu Kocha Mkuu huyo alisema anajivunia kuwa na timu yenye wachezaji vijana na wenye nguvu wanaoweza kukabiliana na mikiki mikiki ya mashindano hayo kutokana na kuwapa mazoezi ya kutosha na lengo la kuandaa vijana hao ni kutwaa ubingwa na kuipandisha timu yeake ili kucheza ligi daraja la kwanza.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake katika uwanja wa ndani wa Jamhuri hapa na mwandihsi wa habari hizi Kocha mkuu huyo Argentina Daudi alisema lengo kuu walilojiwekea pamoja na uongozi mzima wa timu hiyo ni kuhahakisha inapanda daraja na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo kwani uwezo wa kufanya mambo hayo mawili wanayo huku akijivunia kuwa na wachezaji wenye vipaji vya mchezo huo ambao unashika kasi kwa kujizolea mashabiki.

“kwanza JKT Ruvu ina wachezaji ambao wapo tayari kwa ajili ya mashindano haya na tumefanya mazoezi ya nguvu kambini na tumeweza kucheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvuy na timu bora kabisa iliyopo katika ligi daraja la kwanza ya Filbert Bayi lakini katika mchezo huo tulipoteza nasi tumepata faida kwa kusawazisha makosa ambayo yalikuwepo kipindi cha nyuma na sasa tupo tayari kwa mashindano haya”. Alisema Daudi.

Kocha huyo alisema kuwa kikosi chake kiko imara na kitu ambacho anajivunia ni kuwa na wachezaji wazuri walio katika kiwango cha juu cha mchezo huo hasa kwa kutegemea safu yake ya ulinzi ambayo ina uwezo na kuzuia washambuliaji kutoka timu pinzani kutoleta madhala kwenye lango lao ambapo aliwataja kuwa ni Zainabu Rukindo na Anna Masaga huku safu ya washambuliaji ikiongozwa na Mary Bayo na Jawa Iddy ambao washambuliaji hao wakipokea mipira kutoka kwa kiungo tegemeo wa timu hiyo Angela Anold kuwalisha mipira ili kuweza kutumbukiza mpira kwenye nyavu.

Katika mashindano hayo timu ya JKT Ruvu itafungua panzia ya michuano hiyo katika mchezo wa pili dhidi ya timu ya akinadada wa Halmashauri ya Tandahimba kutoka mkoani Mtwara huku timu ya Hamambe inayomilikiwa na Halmashauri ya jiji la Mbeya yenyewe ndiyo itakata utepe kwa mchezo wa kwanza kwa kuvaana na wenyeji timu ya Alance One ambayo yenyewe ikiwa na maskani yake katika kijiji ch Kinglwira ambayo yanaendelea kwenye uwanja wa ndani wa Jamhunri mjini hapa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: