JUMLA YA WASANII 13 WA KUNDI LA TAARABU LA FIVE STAR WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO MARA BAADA YA BASI NDOGO T 351 BGE WALILOKUWA WAKISARIA KUTOKA MBEYA KUELEKEA JIJINI DAR ES SALAAM KUPATA AJALI KATIKA BARABARA KUU YA IRINGA- MOROGORO KWENYE HIFADHI YA MIKUMI NATIONAL PARK KUPINDUKA NA WATU 13 KUJERUHIWA WAKATI DEREVA WA BASI HILO NDOGO AKIJARIBU KULIKIKWEPA LORI T 559 BDL LILILOKUWA LIMEHARIBIKA NA KUEGESHWA KANDO YA BARABARA HIYO.
KATIKA TUKIO LA AJILI HILO PIA ILIHUSISHA NA LORI LINGINE T 530 BHY AMBALO LILIKUWA LIKITOKEA JIJINI DAR ES SALAAM KUGONGA NA BASI HILO NDOGO AMBAPO LILISABABISHA WATU 13 KUFARIKI DUNIA AMBAYO INADAIWA ILITOKEA MAJIRA YA SAA 2:30 MACHI 21 USIKU KATIKA HIFADHI HIYO JIRANI NA KIJIJI CHA DOMA KILICHO JIRANI NA HIFADHI HIYO MKOANI HAPA.
KWA MUJIBU WA MUIMBAJI WA KUNDI HILO LA FIVE STAR MWANAHAWA ALLY (58) WAKATI AKIONGEA NA BLOG HII KATIKA WARD NO 3 YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO ALIKUKOWA AMELAZWA NA WENZAKE ALISEMA KUWA AJALI HIYO ILITOKEA BAADA YA DEREVA WA BASI LAO KUENDESHA GARI PASIPO KUWA NA UANGALIFU NA KUTOKUWA MAKINI JAMBO AMBALO LIMECHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KUTOKEA KWA AJALI HIYO ILIYOSABABISHA UPOTEVU WA ASILIMALI WATU KUFARIKI DUNIA.
MWANAHAWA ALISEMA LORI AMBLO LILIKUWA LIMEEGESHWA KANDO YA BARABARA HIYO AMBALO LILIHARIBIKI WAHUSIKA WAHAKUWEKA ALAMA YO YOTE YA KUASHILIA KUWEPO KWA GARI LILILOHARIBIKA NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HIYO KUCHUKUA TAHADHALI PINDI WANAPOKARIBIA ENEO HILO LILILOHARIBIKA LORI HILO.
WASANII WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA JALI HIYO NI OMARI TALL, ISSA KIJOTI, HAJI BABU, SHEBA JUMA, OMARY HASHIM, TIZO MGUNGA NA HAMISI MIPANGO.
WENGINE WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO NI HUSNA MAPANDE, SAMIL MAULID, HASSAN NGELEZA, KITU TIGO (AMINA) RAMA KINYOYA NA NASSORO MADENGE.
MAJEREHI KATIKA AJALI HIYO NI ALLY JEY. ZENA MOHAMED, MWANAHAWA ALLY (58) SAMILA RAJABU, RAJABU KONDO, BI MWANAHAWA HAMISI (36) NA ISSA MAMONGO.
WENGINE WALIOJERUHIWA NI MIFUPA, SALUM FERUZI. SUZANA BENEDICT, MUSSA, KITU TIGO (MWANZANI ALLY) NA HAMA KIU.
AIDHA BLOG HII HADI MAJIRA YA SAA 12 MCHANA ILISHUHUDIA MAJERUHIWA WATATU WAKIWA KATIKA HOSPITA HIYO BAADA YA WENGINE KUPATA HUDUMA NA KURUHUSI ISIPOKUWA MWANAHAWA ALLY (58), MWANAHAWA HAMISI NA MWANZANI ALLY (KITU TIGO) NA BLOG HII ILIPATIWA TAARIFA ZA KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MUHIMBILI KWA AJILI YA UCHUNGUZI ZAIDI WA AFYA YAKE KUTOKANA NA KUUMIA VIBAYA KATIKA AJALI HIYO.
UONGOZI NA WADAU WA BLOG HII MKOANI MOROGORO TUNAUNGANAN NA FAMILIA ZA WAFIWA NA MAJERUHI KUWAOMBEA MAREHEMU KWA MWENYEZI MUNGU AWALALE MAHALA PEMA POPONI NA KUWAFANYIA UWEPESI MAJERUHI WAWEZE KUPONA HARAKA NA WAREJEE KATIKA MAJUKUMU YAO YA KUJENGA TAIFA.
AMINA.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment