BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RADI YAUA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA MORO VIJIJINI

JUMLA ya watu wane wamefariki dunia papo hapo wakiwemo na wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza kupiga na radi katika shule ya sekondari ya Malengwelengwe iliyopo kata ya Mngazi Tarafa ya Bwakila Chini na wengine 17 kujeruhiwa katika wilaya ya Morogoro Vijijini mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Said Mwambungu alisema tukio hilo lilitokea machi 24 mwaka huu katika kijiji hicho wakati wanafunzi hao wakiwa shule na kubaini tukio la mwanmke mmoja kuliwa na mamba akiwa shambani kwake.

Mwambungu alisema aliwataja wanafunzi waliopoteza maisha katika tukio kuwa ni Abdalah Kibwe (15), Kunambi Adolph (14) na mmoja aliyefahamika kwa jina moja Ambias (15) wote wanaosoma kidato cha kwanza katika shule hiyo ya sekondari ya Malengwelengwe katika kijiji hicho cha Bwakila Chini.

Mkuu huyo alisema kuwa kati ya wanafunzi 17 wawili kati yao hali zao ni mbaya na wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu zaidoi wakati waliosalia walitibiwa kwenye zahanati ya Mngazi na kituo cha afya Dutumi na kuruhusiwa kuendelea na majukumu mengine.

Mwambungu alisema wanafunzi hao walijeruhiwa na radi wakiwa shuleni baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na radi kuanza kunyesha kwa wakati mmoja katika eneo hilo na kwamba baadhi walikuwa madarasani na wengine walikuwa kwenye viwanja vya michezo wakijiandaa na maandalizi kwa mashindano ya UMISETA kwa shule za sekondari yanayotarajia kuanza hivi karibuni.

Katika tukio la pili Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mama Salma Rashid Madenge mkazi wa kijiji cha Lukurunge kata ya Mvuha amefariki baada ya kuliwa na mamba akiwa shambani kwake usiku na mumewe kulinda mazao yasiliwe na wanyama waharibifu.

Mwambungu alisema mwanamke huyo wakiwa na mumewe shambani, ghafla alitokea mamba na kumkamata mwanamke huyo, ambapo mwanaume huyo alifanya jitihada za kukabiliana na mamba huyo na kushindwa baada ya kuzidiwa nguvu na mnyama huyo na kufanikiwa kumuingiza kwenye bwawa lililokaribu na shamba lao.

Alisema mwanaume huyo alipiga kelele za kuomba msaada ambapo walitokea wananchi na kuanza kumsaka mambo huyo lakini jitihada zao ziligonga mwamba, baada ya mamba na kiboko kuonesha ushirikiano wa hali ya juu kwa kutoka ndani ya bwawa hilo na kukabiliana na wananchi hao.

Aidha Mwambungu alimwagiza Afisa Maliasili wa Wilaya kwenda katika eneo hilo ili kuutafuta mwili wa mawanake huyo na kuukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Hata hivyo amewaomba wakazi wa maeneo hayo yaliyopatwa na maafa, kutokuwa na fikira na imani potofu juu ya vifo vya watu hao, na kuwaasa kuona kuwa ni jambo ambalo lilipangwa na mungu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: