BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PAKA MWENYE UNGO NA NGUO NYEUSI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA TUKIO LA USHRIKINA KUSHINDIKANA MORO.

PAKA mwenye ungo na nguo nyeusi amefariki dunia papo hapo baada ya kudondoka kutoka kwenye paa ya nyumba ya mkazi wa mtaa wa Mwembeni kata ya Chamwino,Amina Ally (55) ambapo tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio Mganga wa tiba za asili kutoka mkoa wa Tabora, Mfaume Ally alisema Tukio hilo limetokea machi 30 mwaka huu majira ya saa 10 afajili katika Manispaa ya Morogoro.

Mfaume alisema paka mwenye ungo na nguo nyeusi alidondoka katika nyumba ya mteja wake na kufariki dunia papo hapo baada ya jaribio la kudhulu kwa njia za giza kushindikana kutokana na nyumba hiyo kuwa na kinga.

Alisema kuwa paka huyo licha ya kuwa na ungo na nguo nyeusi (kaniki ambayo alifungwa katika tumbo la paka huyo) alikuwa na vitu vingine vikiwemo salafu za senti tano na senti 10 fedha ya zamani ya Tanzania zilichomekwa kwenye ungo huo huo pamoja na chupa nyekundu akiwa imefungwa katika ukingo wa ungo.

“paka huyu amefariki dunia baada ya jaribio la kudhulu kaya ya nyumba ya mteja wangu Amina Ally kushindikana kutokana na nyumba hii kuwa na kinga na imani za ushirkina, Alisema Ally.

Mganga huyo alisema kuwa mwaka 2009 mteja wake huyo Amina Ally (55) alimweleza kusumbuliwa na matukio yanayohusishwa na imani za ushirikina wakati wa usiku kwenye nyumba yake na baada ya kutumia utalaam wake aliweza kutoa vitu vibaya na ilipokamilika kazi hiyo aliweza kuweka kwa ajili ya kinga.

Naye mmilikiwa wa nyumba hiyo Amina Ally alisema wakati tukio hilo linatokea majira ya saa 10 hakuwepo nyumbani lakini kumekuwa na matukio yanayohusika moja kwa moja na mambo ya ushirkina kwa muda mrefu nyakati za usiku jambo ambalo amekuwa akiishi kwa mashaka kutokana na matukio hayo.

Aidha mmiliki huyo Amina Ally alisema kuwa mwaka 2009 kabla ya kuhamia kwenye nyumba hiyo kulitokea tukio la ajabu la kuonekana kwa paka mwenye umri mdogo ambaye alikanyagwa na mmoja wa wapangaji wake na baada ya kukanyagwa paka huyo alipotea katika mazingira ya kutatanisha ambapo mpangaji huyo mguu wake kulia ulipoteza nguvu za kutembea.

Athibitisha kwa tukio hilo Balozi wa mtaa wa Mwembeni kata ya Chamwino mjini hapa, Abdu Ng’ombe (82) alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 alfaji machi 30 mwaka huu kwenye nyumba ya Amina Ally baada ya kushuhudia kwa kuona paka mwenye ungo ambao ndani yake ulikuwa na salafu za senti tano, senti 10 na salafu ya fedha za kenya, nguo nyeusi (kaniki), chupa nyekundu na nyoya moja nyeupe ya kuku.

Alisema kuwa tukio hilo ni mara yake ya kwanza kuonekana kwenye mtaa huo licha ya kuwepo kwa matukio yanayohusishwa na imani za kishirikina kwa siku za nyuma.

Katika tukio hilo wakazi wa kata Chamwino na kata ya Kiwanja cha Ndege walimiminika kwenye nyumba hiyo kwa lengo la kushuhusia kuona paka huyo ambaye alikuwa na nyungo na nguo nyeusi kuvuta hisia za watu mwengi mjini hapa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: