BAADA YA KUMALIZIKA KWA UCHAGUZI MKUU 2010 YALIJITOKEZA HAYA.
KUTOKA GAZETI LA TANZANIA DAIMA: DK Slaa alishinda urais kwa 64%
Dk Willbrod Slaa ndiye alieshinda kwa kiti cha urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchanguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu Tanzania Daima limeelezwa.
Taarifa za kuaminika kutoka kwa vigogo wa idara hiyo ya usalama waTaifa zinasema Dk Slaa aliekuwa akiwania kiti cha hicho kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alishinda uraisi kwa kuzoa asilimia 64ya kura zote zilizopigwa kwa nafsi hiyo lakini kwa makusudi matokeo halali yalichakachuliwa kumpa ushindi Jakaya Kikwete wa chama cha Mapinduzi (CCM).
Mtoa taarifa wetu kutoka ndani ya idara hiyo amelithibitishia gazeti hili kuwa mbali na kujizolea asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa Dk slaa aliongoza kwa kupata kura nyingi kwenye mikoa 10 dhidi ya kikwete alieongoza kwa kura chache katika mikoa iliyosalia.
Katika matokeo hayo yaliyovujishwa ndani ya siku tatu zilizopita inadaiwa kuwa kikwete alipata asilimia 27 tu ya kura zote zilizopigwa kwa nafasi hiyo ya urais huku asilimia 9 ya kura hizo ikienda kwa vyama vingine kikiwemo chama cha wananchi (CUF). Taarifa hizo ziliendelea kuwa matokeo ya urais yalibadilishwa katika hatua ya ujumlishaji wa kura kwenye majimbo mbalimbali ambapo pale Dk Slaa alipoongoza kwa kura nyingi sana kura hizo zilikuwa zikipunguzwa ili kukaribiana na zili za kikwete.
“unajua kura hazikuibiwa vituoni, matokeo ya vituo karibu yote yalikuwa halali.
Kura ziliibiwa katika majumlisho jimboni na na kwenye majumlisho yaliyofanywa na tume.
Na walitumia udhaifu wa mawakala wa chadema katika majumuisho kuhangaikia zile za ubunge tu na kujisahau kwenye urais. Kama wangekuwa makini katika majumuisho ya urais, maeneo mengi matokeo yasingebadilishwa sana.
” alisema kigogo mmoja wa usalama wa taifa kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Matokeo zaidi ya urais yanaelezwa yalichakachuliwa katika majumlisho ya mwisho ya kura nchi nzima ambapo tume ya taifaya uchanguzi (NEC), inadaiwailipunguza kura za Dk Slaa hata zile zilizokuwa zimeshudiwa kwa pamoja na mawakala wa vyama vya pinzani.
“Mfano wa majimbo ambayo kura zake zilibadilishwa dakika za mwisho na tume ni Ubungo, Musoma mjini, Mbeya mjini, Arusha mjini, Ilala, kawe, Geita, Kilombero, Moshi mjini, Tarime na Songea mjini…” Taarifa zaidi za matokeo hayo ya urais yanayodaiwa kuwa ndiyo halali na sahihi badala ya yale yaliyotangazwa na NEC, zilivujishwa na vigogo wastaafu wa usalama wa taifa ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini.
Hata hivyo, usalama wa Taifa ulikanusha vikali kuhusika katika kuchakachua matokeo ya urais mara baada ya Dk Slaa mwenyewe kutoa malalamiko yake kupitia vyombo ya habari
0 comments:
Post a Comment