BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANASIASA KUKUMBWA NA MIKOSE UTABIRI WA SHEKH YAHAYA


MTABIRI maarufu Afrika Mashariki na Kati, Shekhe Yahya Hussein, amesema baadhi ya viongozi na wafanyabiashara maarufu nchini kuwa wengi wao watatekwa na kuporwa mali zao na kwamba matukio hayo yatafanyika kati ya mwezi huu na Julai mwaka huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Shekhe Hussein aliwataka viongozi na wafanyabiashara hao, kuchukua tahadhari katika shughuli zao na hasa katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao wanapaswa kujichunga ili wasitekwe, wasiibiwe mali zao na kufanywa bidhaa."Kuanzia April 19 na kuendelea hadi Julai viongozi wa vyama vya siasa na wafanyabiashara maarufu, wajichunge ili kuepuka kutekwa nyara na kuibiwa na hata wao wenyewe kufanywa kama bidhaa," alisema Shehe Yahaya.

Alisema kwa kipindi hicho viongozi hao wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa hasa katika matembezi yao ya kila siku.Alisema utekaji nyara huo dhidi ya watu waliotajwa, utafanyika wakiwa safarini au kwenye mikutano na kwamba ni vizuri wasiwe peke yao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: