BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAHINSANO YA MEI MOSI KUFIKA TAMATI APRIL 29 MORO.


WACHEZAJI WA TIMU ZA NETIBOLI WAKICHUNA KATIKA MCHEZO WA NUSU FAINALI KATI YA IDARA YA POLISI NA MABO YA NDANI.

MASHINDANO ya Mei Mosi yanatarajia kufikia tamati April 29 baada ya kumalizika kwa michezo tofauti ya fainali katika uwanja wa Jamhuri kuanzia majira ya saa 8 mchana katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Akizngumza na gazeti hili Katibu wa Kamati ya Michezo Mei Mosi Taifa Award Safari alisema mashindano ya Mei Mosi mwaka 2011yanatarajia kufika tamati baada ya kumalizika kwa michezo mitatu tofauti baada ya timu za michezo hiyo kufanikiwa kuingia hatua ya kucheza fainali kuanzia majira ya saa 8 mchana kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Safari alianza kwa kutaja timu za soka zilizofanikiwa kuingia hatua ya kucheza fainali baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali kuwa ni timu ya Ulinzi Sport Club iliyoingia fainali baada ya kuifunga timu ya Idara ya Polisi kwa pinde kwa changamoto ya mikwaju ya penalti kwa bao 5-4 kufuatia kumalizika kwa dakika 120 za mchezo huo kushindwa kufungana katika dakika za kawaida ndipo ilipotumika kanuni za mchezo huo kupiga penalti baada ya kumalizka kwa dakika za nyingeza kushindwa kumpata mshindi.

Huku timu ya Tumbaku Fc ikifanikiwa kucheza fainali baada ya kuitandika timu ya Alliance katika mchezo wa nusu fainali kwa bao 4-1. Alisema Safari.

Kwa upande wa mchezo wa netiboli timu ya Idara ya Polisi ilifanikiwa kucheza fainali kwa ushindi mabao 48-47 dhidi ya mahasimu wao wakubwa katika mchezo huo timu ya Mambo ya Ndani ikiwa ni tofauti ya bao moja ambapo ililazimika kuongeza muda wa nyinmgeza ili kumpata mshindi kwa kuongeza dakika saba ambazo ziliamua mshindi wa mchezo huo ambao Idara ya Polisi iliibuka mshindi kutokana na kumalizika kwa mchezo wao na matokeo kuwa sare ya mabao 37-37.

Aidha Safari alieleza kuwa katika mchezo wa kuvuka kamba kwa wanaume timu ya Mahakama ilifakikiwa kutinga fainali ili kuchuana na timu ya Uchukuzi baada ya kuishindi timu ya Hazina kwa ushindi wa 2-0 huku timu ya Uchukuzi nayo ikiwatoa timu ya Idara ya Polisi kwa ushindi wa 2-0.

katika upande wa akinadada katika mchezo huo wa kuvuta kamba timu ya Mahakama nayo imeingia fainali baada ya ushidni wa ushindi wa 2-0 dhid ya Afya huku timu ya Uchukuzi ikiwatupa ikiingia katika hatua ya kucheza fainali kwa ushindi Maliasili kwa ushidni wa 1-0.

Safari alisema kuwa baada ya kupatikana kwa washindi wa kwanza kwa michezo mingine kivumbi cha mashindano ya Mei Mosi kinatarajia kufikia tamati April 29 katika uwanja huo wa Jamhuri baada ya kumalizika kwa timu zilizofanikiwa kucheza michezo ya fainali.

Pia alimetoa wito kwa wachezaji wa timu zilizoshiriki michuano hiyo kufika katika uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 8 mchana ili kuzishangilia timu ambazo zitacheza michezo yao ya fainali ikiwa ni kutoa hamasa kwa timu hizo kwani michezo ni furaha na upendo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: