MASHINDANO YA MEI MOSI YASIKA KASI KWA MORO.
MSHAMBULIAJI WA TIMU YA SOKA YA IDARA YA POLISI MWINYIJUMA JUMBE KUSHOTO AKIWANIA MPIRA DHIDI MLINZI WA TIMU YA UKAGUZI SPORT CLUB ALFONCE SIKA KUSHOTO WAKATI WA MASHINDANO YA MEI MOSI YANAYOENDELEA KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO AMBAPO MCHEZO HUO ULIMALIZIKA KWA UKAGUZI KUFUNGWA KUFUNGWA MABAO 6-3.
TIMU ya soka ya Ukaguzi Sport Club imeendeleza wimbi la kupoteza matumani ya kusonga katika michuano ya Mei Mosi baada ya kukubali kipigo cha tatu mfululizi kutoka kwa timu ya Idara ya Polisi kwa bao 6-3 mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Katika michuano hiyo timu ya Ukaguzi Sport Club tayari wamepoteza michezo yake miwili kati ya Mabingwa wa mkoa wa Morogoro timu ya Tumbaku Fc kwa kupokea kichapo cha bao 4-3 kabla ya kufungwa na timu ya Ulinzi kwa bao 5-1.
Timu ya soka ya Idara ya Polisi Fc ilianza mchezo huo kwa kasi huku safu ya ushambuliaji ikicheza kwa umakini na kulifikia lango la wapinzani wao ambapo katika dakika ya nane mshambuliaji, Mokili Lambo aliiandikia timu yake bao la kuongoza baada ya mlinzi wa Ukaguzi Masoud Seleman kufanya madhambi eneo la hatari na mwamuzi Hamis Kambi kutoa adhabu hiyo.
Mshambuliaji Imani Mapunda wa timu ya Idara ya Polisi alifunga mabao mawili dakika ya 26 na dakika ya 38 huku mshambuliaji Nicolaus Kabipe akifunga bao la nne katika daika ya 18.
Huku mshambuliaji Mokili Lambo akipachika mabao mengine mawili katika dakika ya 47 na dakika 49 na kukamilisha idadi ya ushindi mnono wa bao 6-3.
Wakati mabao ya timu ya Ukaguzi Sport Club yakipatika katika dakika ya 43 na 50 yakipachikwa wavuni na mshambuliaji Ridhaa Abeid huku bao la tatu likifungwa na Ally Saidi dakika ya 57.
Matokeo ya michezo mingine timu ya Alliance One ilitoa dozi kali kwa timu ya Mipango kwa kuitandika mabao 5-0.
Wakati katika michezo ya netiboli timu ya akinadada wa Alliance One iliweza kuifunga timu ya Ukaguzi kwa bao 21-17 kabla ya Uhamiaji nayo ilifanikiwa kuwalaza timu ya Maliasili kwa bao 45-16.
Mzinga ilipata ushindi dhidi ya timu ya Utumishi kwa kuwafunga bao 27-7 na Ras Rukwa iliitaandika timu ya Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) kwa kuifunga mabao 23-21.
0 comments:
Post a Comment