ULINZI SPORT CLUB YATOA DOZI DHIDI YA UKAGUZI MASHINDANO YA MEI MOSI MOROGORO.
Mshmbuliaji wa timu ya Ulinzi Sport Club Saidi Seif kushoto akimtoka mlinzi wa timu ya Hazina Fc Ahmada Kombo wakati wa mashindano ya Mei Mosi katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo Hazina Fc ilishinda kwa bao 2-1.
TIMU ya soka ya Ulinzi Sport Club imetoa kipigo kikali katika michuaano ya Mei Mosi baada ya kuiadhibu timu ya Ukaguzi Fc katika muendelezo wa michezo hiyo kwa kuitandika bao 5-1 uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Vijana wa timu ya Ukaguzi ndiyo walionza kupata bao katika dakika ya 18 baada ya mshambualia wao tegemeo Ridhaa Abeid kupiga mpira uliomshinda mlindamlongo wa timu ya Ulinzi Sport Club na kuiandikai timu yake bao la kuongoza.
Baada ya kuingia kwa bao hilo timu ya Ulinzi Sport Club ilianza kulisakama lango la wapinzania wao na katika dakika ya 25 Charles Nolbert aliisawazishia timu yake kwa kufunga bao hilo.
Kufuatia kupata bao hilo timu ya Ulinzi Sport Club ilizidisha mashambulizi kwa timu ya Ukaguzi mfululizo na dakika ya 46 waliweza kupata bao la pili lililofungwa na Lucas Saimon kufuatia safu ya ushambuliajia wa timu hiyo kuonana vizuri katika eneo la hatari na kutoa pasi kwa mfungaji kuandika bao hilo.
Katika mchezo huo timu ya Ukaguzi ilionekana kuzidiwa uwezo hasa katika idara ya kiungo na ulinzi hali iliyowapa mwanya washambuliaji wa timu ya Ulinzi Sport Club kutawala maeneo hayo na kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambapo kwenye dakika ya 63 kiungo Libertus Manyasi aliifungia timu yake bao la tatu.
Timu ya Ulinzi Sport Club iliendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango la wapinzani wao hali hiyo iliwafanya wabeki wa Ukaguzi kutoa mwanya kwa mshmbauliaji Paul Ndauka kuiandikia timu yake ya Ulinzi Sport Club kufunga bao la nne dakika ya 68 katika mchezo huo.
Mshaambuliaji Lucas Saimon aliweza kufunga kalamu ya mabao kwa timu yake ya Ulinzi Sport Club kwa kufunga bao la tano ikiwa bi bao lake la pili kwenye mchezo huo ambalo alifunga kwenye dakika ya 89 kufuatia kutokea mpira ambao mabeki wa Ukaguzi walizembea kutoa katika eneo la hatari kabla ya mfungaji kufunga bao hilo na kufanya matokea kuwa 5-1.
Katika mchezo mungine timu ya Uchukuzi Sport Club iliweza kuibuka na ushindi mwembamba dhidi yaa timu ya Maliasili Fc kwa kuifunga bao 2-1 kwenye uwanja huo wa Jamhuri mjini hapa ambapo michezo mingine inaendelea.
0 comments:
Post a Comment