WASHINDI wa kwanza kwa michezo mitano tofauti ikiweno mchezo wa jadi wa bao, draft,mbio za baiskeli na riadha wamepatikana baada ya kufanyika kwa michezo hiyo ya mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro jana.
Akizungumza na gazeti hili katika uwanja wa Jamhuri mara baada ya kumalizika kwa michezo hiyo Katibu Msaidizi Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, Joyce Benjamin alisema kulikuwa na jumla ya michezo mitano tofauti kwa washiriki kushindana kutafuta mshindi wa kwanza hadi wa tatu katika michezo ya bao, karata, draft, mbio za baiskeli na riadha.
Alisema kuwa washindi wa michezo hiyo baada ya kupatikana watakabidhiwa zawadi za vikombe na Rais Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za mei mosi zitakazofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Benjamin alianza kwa kuwataja washindi wa kwanza akianzia na mchezo wa riadha kwa wanaume kuwa ni Satnley Asenga wa Uhamiaji ambaye alitumia muda wa dakika 22:12.48 wakati mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Flora Odilo wa Tamisemi aliibuka mshindi baada ya kutumia muda wa dakika 34:30.52 katika mbio za mchezo huo za kilometa 10 ambapo walizunguka mara 12 na nusu uwanja wa Chuo cha Kiislam (zamani tenesco mjini hapa.
Katika mchezo wa baiskeli mshindi wa kwanza wanaume Abdallah Okumu wa Maliasili aliwashinda washikiri wenzake katika mbio hizo kwa kumaliza akitumia muda wa dakika 24:9.9 huku upande wa wanawake Donesia Tesha wa Hazina alishinda na kuibuka mshindi wa kwanza kwa kumaliza muda wa dakika 32:.5.4 alisema Benjamin.
Aliendelea kutaja washindi wa kwanza katika michezo mingine kuwa Saidi Kachonjo wa Mzinga alimshinda Kana Jongo wa Maliasili katika mchezo wa fainali kwa ushindi wa bao 2-1, wakati kwa upande wa wanawake kwa mchezo huo wa bao Elizaberth Jonathan alifanikiwa kushinda dhidi ya mpinzani wake Thea Samjela kwa bao 2-1.
Washindi wengine ni Sanley Martin wa Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) alibuka mshindi kwanza huku upande wa wanawake Mackhiyo Katua aliibuka mshindi wa kwanza, katika karata Stanford Busumbilo kutoka Mambo ya Ndani alitawazwa mshindi wa kwanza na Mwanaidi Omari wa CDA Dodoma naye alibuka na ushindi kwa upande wa mchezo huo. Alisema Katibu huyo Msaidizi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment