MTOTO Juma Salum (2) mkazi wa kijiji cha Nyangabu kata ya Nguruka wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma anahitaji msaada wa kiasi cha sh 750,000 ili aweze kufanikisha zoezi la upasuaji tundu la haja kubwa baada ya kuzaliwa bila kuwa na sehemu hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa, babu wa mtoto huyo, Hamisi Jumanne (56) mkazi wa Kihonda katika Manispaa ya Morogoro alisema mtoto huyo anahitaji upasuaji huo baada ya kuzaliwa bila ya kuwa na sehemu za haja kubwa.
Jumanne alisema kutokana na kukosekana kwa sehemu hiyo kumesababisha mtoto huyo kupata haja kubwa kwa kutumia sehemu zake za ziri na hivyo kupata maumivu makali sambamba na kutoa kilio wakati wa kutoa haja hiyo.
Babu wa mtoto huyo alibainisha kuwa mtoto huyo anahitaji kufanyiwa upasuaji mei 5 mwaka huu kwenye ya hospitali ya rufaa ya Kilimanjaro Christian Medical Centre KCMC na kwamba kiasi hicho kinatakiwa ili kuwezesha kufanyiwa upasuaji huo.
Alisema familia yake ina kipato cha chini hali ambayo imepelekea kushindwa kumudu gharama hizo na hivyo kulazimika kuomba msaada kwenye Taasisi za Serikali, watu binafsi na Mashirika ya Dini ili aweze kupata fedha hizo za matibabu ya mtoto huyo.
Kwa Upande wa baba wa mtoto huyo, Salum Juma (38) ambaye kwa sasa yupo mkoani hapa alisema kuwa mtoto huyo aligunduliwa kuwa na tatizo hilo baada ya siku tatu tangu kuzaliwa kwake kufuatia kukosa choo na kwamba ameamua kuja mkoni hapa kuomba msaada kwa ndugu na jamaa.
“mke wangu ndiye alikuwa wa kwanza kugundua kuwa mtoto wetu hana sehemu ya haja kubwa baada ya kukaa naye kwa siku tatu tangu kuzaliwa kwake kushindwa kuona choo jambo ambalo lilimtia wasiwasi na kunieleza mimi juu ya hali hiyo.” Alisema
Alisema walifunga safari yeye na mke wake ya kwenda katika Zahanati ya Kijiji cha Nguruka alipozaliwa mtoto huyo kwa ajili ya uchunguzi wa awali na kwamba Daktari wa Zahanati hiyo aligundua mtoto huyo kukosa sehemu hiyo na kuwaandikia barua ya kwenda katika hospitali ya Nkinga Mission ya mkoani Tabora kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Alifafanua kuwa baada ya kufika katika hospitali hiyo Madaktari walimfanyia uchunguzi na kubaini tatizo hilo ambapo walimfanyia upasuaji wa muda na kumwezesha haja kubwa kutoka sehemu ya ubavu wa kushoto sambamba na kumpa kifaa maalum cha kuhifadhia uchafu na kudumu nacho kwa muda wa majuma mawili.
Alisema kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo alirudi nyumbani na baada ya wiki mbili kifaa hicho maalum kilitolewa na kupewa barua ya kwenda katika hospitali ya rufaa ya Bugando mkoani Mwanza ambako alifanyiwa upasuaji tena na kuongezwa tundu ubavu ili kuwezesha uchafu wa haja kubwa kutoka kwa urahisi zaidi.
Hata hivyo alisema baada ya kurudi katika hospitali ya Bugando Mwanza kwa mara ya pili madaktari hao waliwapatia barua ya rufaa ya kwenda (KCMC) kwa upasuaji wa tundu la haja kubwa ambapo walifanyiwa upasuaji huo na kutakiwa kurudi kwa mara nyingine ili utumbo wa haja ndogo na kubwa uweze kurudishwa kwenye mfumo wa kawaidi.
TUNAWEZA KUCHANGIA FEDHA KWA NJIA YA M.PESA NK ILI MTOTO HUYO AWEZE KUPATIWA HUDUMA YA UPASUAJI WA AWAMU YA MWISHO PALE KCMC MEI 05 MWAKA HUU KWA NAMBA ZA SIMU YA MKONONI HAPA CHINI.
0687 11 71 25.
0659 79 06 14.
0716 95 63 46.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment