TIMU ya netiboli ya idara ta Polisi imetinga nusu fainali baada ya kuilaza timy ya Alliance One katika mchezo war obo fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri kwa mabao 53-10.
Wakitumia udhaifu wa wachezaji wa timu ya Alliance One kupoteza mipira wakati wa mchezo huo iliwapa mwanya wachezaji wa timu ya Idara ya Polisi kutawaala sehemu kubwa ya mchezo huo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.
Timu ya Idara ya Polisi ikiwatumia wafungaji wao hodari tegemeo, Fatuma Chanzi ambaye alifanikiwa kufunga jumla ya mabao ya 29 huku Aziza Itonya naye alifunga jumla ya 24 huku timu ya Alliance One ilifanikiwa kufunga bao 10 kuptia wafungaji wao Vida Mango alifunga jumla ya bao 9 huku Mariam Juma akifunga bao moja katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa timu ya Idara ya Polisi kushinda 53-10 dhidi ya Alliance One.
Katika michezo mingine ilichezwa katika uwanja huo timu ya Mambo ya Ndani iliishinda timu ya akinadada wa Tumbaku kwa ushindi wa bao 37-16, huku timu ya Uhamiaji nayo iliilalua timu ya Ras Dodoma kwa ushindi wa bao 38-25 na timu ya CDA iliishinda kwa taabu timu ya akinadada wa Iadra ya Afya kwa kuwafunga bao 18-15.
Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Anna Kibila alitaja timu zilifuzu baada ya kumalizika kwa michezo ya robo fainali na kujulikana timu zilizoingia kucheza nusu fainali ya michuano hiyo kwa upande wa netiboli ni timu ya wizara ya Mambo ya Ndani itapambana na timu ya Idara ya Polisi huku timu ya Uhamiaji ikitarajiwa kucheza na timu ya CDA ya Dodoma april 27 kwenye uwanja huo wa Jamahuri mjini hapa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / TIMU YA IDARA YA POLISI NETIBOLI YATINGA NUSU FAINALI BAADA YA KUTOA KIPIGO KIKALI MEI MOSI DHIDI YA ALLIANCE ONE.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment