TIMU za soka za Ulinzi Sport Club na Idara ya Polisi zimefanikiwa kutinga nusu fainali katika mashindano ya Mei Mosi baada ya kupata ushidi mnono dhidi ya wapinzani wao michezo ilifanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Ili timu ya Ulinzi Sport Club iliyotoa kipichapo kwa kuikandamiza timu ya Afya bao 4-0 katika mchezo war obo fainali waakati timu ya Idara ya Polisi nayo ilipata ushindi wa bao 3-1 dhid ya Uchukuzi Sport Club na timu hizo kujihahakishia kucheza nusu fainali katika mashindano hayo.
Timu ya Ulinzi Sport Club ilipata bao la kwanza katika mchezo ddhidi ya Afya kipindi cha kwanza likifungwa na mshambulia Paul Ndauka katika dakika ya pili baada ya kumpiga chenga mlinda mlango wa Saidi Kindamba na mpira kujaa wavuni.
Kipindi cha pili timu ya Ulinzi Sport Club iliongeza mashmbulizi katika lango la wapinzania wao na kufanikiwa kupata mabao katika dakika ya 31 likifungwa na Liberatus Manyasi huku Charles Norbert akiongeza bao la tatu dakika ya 47 kabla ya Lucas Saimon kuandika bao la nne dakika ya 69 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa timu ya Ulinzi Sport Club kuibuka na ushindi mnono dhidi ya timu ya Afya kwa bao 4-0.
Wakati timu ya Idara ya Polisi nayo ilifanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuilaza timu ya Uchukuzi Sport Club kwa mabao ya Iman Mapunda dakika ya 50 huku Salum Bakari aliipatia timu yake bao la pili dakika ya 64 na Silvester Kimeli kupachika bao la tatu huku bao la kufutia machozi la timu ya Uchukuzi Sport Club lilifungwa na Isack Ibrahim dakika ya 56 katika mchezo huo uliomalizka kwa Idara ya Polsi kushinda kwa bao 3-1 dhidi ya timu ya Uchukuzi Sport Club.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment