BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ULINZI SPORT CLUB YATWAA UBINGWA WA SOKA MASHINDANO YA MEI MOSI 2011 MORO.

TIMU ya soka ya Ulinzi Sport Club imetwaa ubingwa wa mashindano ya Mei Mosi baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Tumbaku Fc katika mchezo mkali wa fainali uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kwa bao 2-1.

Mashindano hayo Mei Mosi yamefikia tamati April 29 mwaka huu kwa timu kuhitimisha michezo mitatu tofauti ya fainali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli na kuvuta kamba wanaume na wanawake ambapo michezo hiyo iliyoanza kuchezwa mapema majira ya saa 2 asubuhi kwenye huo wa uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Katika mchezo wa soka timu ya Ulinzi Sport Club ilipata mabao pekee yaliyofungwa na mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Paul Ndauka katika dakika ya 27 na dakika ya 42 na kuihakikishia ushinda huo wa bao 2-1 kwa timu yake na kutwaa ubingwa wa Mei Mosi kwa mwaka 2011.

Mshambulia huo, Paul Ndauka ambaye alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye fainali hiyo aliifungia timu yake bao la kwanza baada ya kuunganisha vema krosi ya Lucas Ladebe na kupiga mpira hafifu uliojaa wavuni huku ukimshinda mlinda mlongo wa timu ya Tumbaku Fc, Rajab Mushi asijuwe la kufanya na bao la pili alifunga kwa kichwa kufuatia kona ilichongwa na Mohamed Ussi na kuukwamisha mpira huo wavuni.

Bao la kufutia machozi kwa timu ya Tumbaku Fc ambao ni mabingwa wa mkoa wa Morogoro lilipatikana dakika ya 70 likifungwa na nahodha wao, Julius Tindwa kwa kichwa baada ya kona iliyopigwa na, Willie Kavuta na kufanya mchezo huo kumalizika kwa timu ya Ulinzi Sport Club kuibuka na ushindi huo wa bao 2-1.

Katika michezo mingine timu ya netiboli ya Mamlaka ya Ustawishaji Mkao Makuu Dodoma (CDA) nayo waliibuka na ubingwa wa mchezo huo wa netiboli katika mashindano hayo ya Mei Mosi baada ya kuitandika timu ya Idara ya Polisi katika mchezo mkali na wakusisimua wa fainali uliofanyika mapema majira ya saa 2 asubuhi kwa ushindi wa jumla ya bao 36-31.

Ushindi wa timu ya CDA ulichangiwa na wafungaji wao tegemeo, Rukia Shabaan aliyefunga jumla ya bao 27 huku Tatu Fungo akifunga jumla ya bao 9 katika mchezo huo wakati mabao ya timu ya Idara ya Polisi yalifungwa na Fatuma Chanzi ambaye alifunga jumla ya bao 19 na Aziza Itonya akifunga jumla ya bao 12.

Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba wanaume timu ya Mahakama iliibuka na bingwa wa mashindano hayo baada ya kufanikiwa kuwavuta wapinzania wao timu ya Uchukuzi katika mchezo wa fainali kwa 2-0 huku wanawake wa timu hiyo ya Mahakama nayo iliwashinda akinadada wa timu ya Uchukuzi kwa ushindi wa 2-0 katika mchezo wa fainali iliyofanyika kwenye uwanja huo wa Jmahuri Morogoro.

Katika mashindano hayo ambayo yalifungwa na mgeni rasmi Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Gratian Mukoba ambapo alitoa zawadi ya vikombe kwa washindi wa kwanza, wapili na watatu kwa michezo minane tofauti ambayo ilifikia tamati april 29 mwaka huu uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: