BONANZA la michezo kwa wanafunzi wenye ulamavu wa akili na viungo limemalizika kwa kupata washindi wa kwanza katika viwanja vya shule ya msingi Bungo mjini hapa.
Mwenyekiti wa bonanza hilo lililozishirikisha jumla ya shule tisa za msingi katika Manispaa ya Morogoro na wanamichezo 200, Mkoba Mkude alimtaja mshindi wa nafasi ya kwanza katika mchezo wa kukimbiza kuku kuwa ni Richard Nyandindi kwa upande wa wavulana kutoka shule ya msingi Kilakala.
Mkude alisema kuwa kwa upande wa wasichana, Janeth Nelson wa shule ya msingi kiwanja cha Ndege alifanikiwa kunyakua kuku baada ya kufanikiwa kumkimbiza na kumkamata jogoo.
Katika mchezo wa kukimbia na gunia, Christopher Keneth wa shule ya msingi Kikundi aliibuka mshinda wa kwanza kwa wanafunzi wenye umri mkubwa na huku kwa wanafunzi wenye umri mdogo,Yasin Saleh wa shule ya msingi Kilakala naye aliibuka mshindi wa kwanza.
Mwenyekiti huyo alisema kwa upande wa mbio hizo za magunia, Pili Hemed wa shule ya Kihonda alishinda kwa wasichana wadogo huku katika mbio za wasichana wenye umri mkubwa Mariam Hemed naye alishinda kwa kushika nafasi ya kwanza.
Alisema katika riadha za umbali wa mita miamoja, Christopher Keneth wa shule ya Kikundi aliibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa wavulana huku Maria Nyoni kwa upande wa wasichana akishinda katika mbio hizo kwa wasichana.
Mkude alisema kuwa kwa upande wa mpira wa kengere kwa watoto wasiona na wenye uoni hafifu timu ya wasichana mchanganyiko waliibuka washindi baada ya kuwafunga wavulana kwa bao 4-3.
Katika upande wa uchoraji Saidi Hamisi wa shule ya Kilakala aliweza kuibuka mshindi wa kwanza baada ya kufanikiwa kuchora vizuri sura ya binadamu katika shindano hilo lililoshirikisha wachoraji watano.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment