BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAFUNZI 200 WENYE WENYE ULEMAVU WA SHULE ZA MSINGI TISA MORO KUSHIRIKI KATIKA BONANZA LA MICHEZO.

JUMLA ya watoto 200 wenye ulamavu mbalimbali wa akili na viungo katika shule tisa za msingi Manispaa ya Morogoro wanatarajia kushiriki katika bonanza la michezo mei 18 mwaka huu katika viwanja vya shule ya msingi Bungo mkoani hapa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika ofisi za gazeti hili mjini hapa, Mwenyekiti wa Michezo wa Vitengo vya Watoto Walemavu Manispaa ya Morogoro, Mkoba Mkude alisema kuwa mei 18 mwaka huu kutafanyika bonanza litakalo jumuisha jumla ya watoto 200 kutoka katika shule tisa za msingi na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo ya Morogoro, Amir Nondo.

Mkude alisema kuwa bonanza hilo litashirikisha jumla ya michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa wavulana, netoboli wasichana, riadha wasichana na wavulana mita 100, mita 200 wavulana na wasichana kupokezana vijiti, kuvuta kamba wavulana na wasichana, kufukuza kuku, kukimbia na magunia na uchoraji wa picha mbalimbali.

Mwenyekiti huyo alitaja makundi ya ulemavu kuwa ni matatu ambayo yatashiriki katika bonanza hilo kuwa ni kundi la watoto walemavu wa akili la shule ya msingi Bungo, Kikundi, Mwembesongo, Kauzeni, Mazimbu na Kiwanja cha Ndege.

Alitaja kundi lingine la pili kuwa ni watoto walemavu wa kusikia (viziwi) shule ya msingi Kilakala, Kihonda Notho, Kiwanja cha Ndege, Kauzeni, na kundi la tatu ni watoto wenye ulemavu wa kuona kuwa ni shule ya msingi Mafiga na kuwa lengo la bonanza hilo ni kuibua vipaji vilivyojifika kupitia watoto hao na kufahamiana kupitia michezo hiyo.

Mkude alisema kuwa katika bonanza hilo kutakuwa na zawadi ndogo ndogo kwa washindi wataofanya vizuri ikiwemo daftari, kalama, penseli na pikipipi.

Mwenyekiti huyo wa Michezo kwa Vitengo vya Watoto Walemavu Manispaa ya Morogoro ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa hiyo na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Bungo ili kuweza kushuhudia michezo hiyo jinsi watoto wenye ulemavu watavyoshiriki katika michezo mbalimbali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: