Mchezaji wa timu ya Mvomero YusuphSaidi (mwenye mpira) akimtoka mchezaji wa timu ya Kilombero Athanas Mdamu huku Mbwana Juma akiandaa kutoa msaada wakati wa mashindano ya copa coca cola ngazi ya mkoa wa Morogoro chini ya umri wa miaka 17 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mcheza huo timu ya Kilombero iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mchezaji wa timu ya wilaya ya Mvomero Rajab Ibrahim kulia akitafuta mbinu ya kumtoka mchezaji wa timu ya wilaya ya Kilombero wakati wa mashindano ya copa coca cola ngazi ya mkoa wa Morogoro chini ya umri wa miaka 17 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mcheza huo timu ya Kilombero iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
TIMU ya soka chini ya umri wa miaka 17 ya Manispaa ya Morogoro (U17) imeanza vema mashindano ya Copa Coca Cola ngazi ya mkoa huo kwa kutoa kipigo kikali dhidi ya timu ya Morogoro Vijijini katika mchezo wa ufunguzi mashindano hayo yaliyoanza kutimua vumbia Mei 2 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa kwa kupata ushindi mnono wa bao 4-o.
Vijana hao wa Manispaa ya Morogoro ilianza kupata ushidi huo kupitia kwa washambuliaji wao tegemeo Basi Abduli aliyepachika mabao matatu nyavuni na Agraham Naftali aliyefunga moja katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na timu ya Manispaa ya Morogoro kwa kila idara.
Mshambuliaji Basil Abdul akitumia uzembe wa mabeki wa timu ya Morogoro Vijijini aliweza kupachika bao la kwanza katika dakika ya 17 baada ya kupokea pasi ya kiungo wa timu hiyo Alfan Mwande wakati bao la pili akifunga dakika ya 43 baada ya kushirikiana vema na Jamali Akida huku bao la tatu akifungwa kwa krosi ya Athman Ally dakika ya70.
Bao la nne la timu ya Manispaa ya Morogoro lilipatikana katika dakika ya 30 likifungwa na mshambuliaji Agraham Naftal baada ya kazi mzuri ya kiungo Alfan mwande kuwatoka mabeki wa Morogoro Vijijini na kutoa krosi iliyomkuta mfungaji kufunga bao hilo na kufanya mchezo huo umalizike kwa timu ya Manispaa ya Morogoro kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-0.
Katika mchezo mungine ambao uliwakutanisha timu ya wilaya ya Mvomero ambao walipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa vijana wa wilaya ya Kilombero huku bao pekee la mchezo huo likifungwa na mshambuliaji Pius Chonesi katika dakika ya 56 baada ya kazi mzuri ya Halidi Hamis kumimina krosi iliyomkuta mfungaji na kuandika bao hilo kwa timu yake ambapo walishidni kwa ushindi huop bao 1-0.
Katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha timu sita za wilaya ya Mvomero, Kilosa, Ulanga, Morogoro, Kilombero na Morogoro Vijijini Katibu Mkuu wa Chama cha mpira wa Miguu mkoa wa Morogoro (MRFA) Hamisi Semka alisema kuwa mashindano hayo yatatumika kuchangua wachezaji wataounda timu ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Copa Coca Cola Taifa yatayofanyika baadaye Jijini Dar es Salaam.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment