BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TUNAKUSIKILIZA KWA UMAKINI.


Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeria kushoto (aliyejishika mikono kifuani) na Afisa wa Maliasili na Mazingira wilaya ya Morogoro Malango Andengenye wa pili (mwenye koti) wakimsikiliza mfanyabiashara Saleh Ufole kulia mara baada ya wananchi kumkamata na kumzuwia kwa madai ya kutaka kusafirisha magogo yanayodaiwa kuvunwa kinyume na sheria za uvunaji wa mazao ya misitu katika msitu wa hifadhi wa Mkulazi uliopo kijiji cha Kiganila kata ya Selembala wilaya ya Morogoro Vijijini mkoani hapa.



MAZAO ya misitu yenye thamani ya zaidi ya sh 10 Mil yamekamatwa na wananchi wa vijiji vya Kiganila na Bwakila Juu baada ya kukiuka sheria za uvunaji wa mazao hayo katika msitu wa hifadhi wa Mkulazi uliopo kata ya Selembala wilaya ya Morogoro mkoani hapa.


Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum mjini hapa Afisa Ardhi Maliasili na Mazingira wilaya ya Morogoro Mlango Andengenye alisema kuwa wananchi wa vijiji vya Kiganila na Bwakila Juu wamefanikisha zoezi la kukamata mazao ya misitu baada ya wavunaji kukiuka sheria za uvunaji wa mazao ya misitu ya hifadhi wa Mkulazi na Bwakila Juu mkoani hapa.

Andengenye alisema wananchi hao kwa ushirikiano wao walifanikiwa kumzuia mfanyabiashara wa mbao, Abdalah Ally kusafirisha mbao 1200 kwenda eneo la Fire Manispaa ya Morogoro baada ya kupasulisha mbao kwa kukiuka taratibu za sheria za uvunaji mbao kijiji cha Bwakila juu ambazo mbao hizo mara baada ya kukamatwa zilihifadhiwa katika ofisi ya mtendaji kata ya Selembala.

Aidha Afisa huyo aliendelea kueleza juu ya wananchi walivyoweza kufanikisha zoezi la ukamataji wa mazao na kuyazuia kuwa katika kijiji cha Kiganila waliweza kumzuia mfanyabiashara, Saleh Ufole kusafirisha magogo kwenda Dar es Salaam baada ya kuvuna magogo 60 kinyume na maelezo yaliyopo kwenye leseni yake ya kuvuna magogo25 .

Andengenye alisema kuwa baada ya wananchi kubaini utoroshaji wa mazao hayo walichukua jukumu la kuwajulisha viongozi akiwemo mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeris, Diwani wa kata ya Salambala, Zuberi Mwenegoha na Afisa Mtendaji wa kata ya Selambala Joseph Ngalawa kwa kuwapigia simu kuwajulisha juu ya tukio hilo ambao walifika katika vijiji hivyo na kuona mazao hayo.

Naye Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeris akizungumzia tukio hilo alisema amewapongeza wananchi wa vijiji hivyo vya Kiganila na Bwakila Juu kwa mwamko waliokuwa nao kwa kubaini mapema wizi na utoroshaji wa mazao ya misitu.

Kalogeris alisema kuwa kama wananchi wamekuwa na mwamko wa kubaini wizi wa mazao ya misitu ipo haja kwa viongozi wahusika nao kufuatilia kwa ukaribu nyendo za wafanyabiasha mara baada ya kuwapatia leseni za kuvuna mazao hayo kwani wengi wao wamekuwa wakitumia mwanya huo wa kutofuatiliwa na viongozi kuiba mali za wananchi kwa kisingizio cha kuwa na kibali.

Pia mbunge huyo alidai kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakinufaika zaidi na utaratibu huo kwani hakuna kiongozi wa kumfuatilia huku baadhi ya viongozi nao wakinufaika na mpango huo na kuwaacha wananchi wakiendelea kutabika.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: