UN YASEMA WATOTO ZAIDI YA 1,300 WA KIPALESTINA WAMEUWAWA NA WAZAYUNI TOKEA MWAKA 2000.
Tume ya Kutetea Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayoonyesha kuwa, hadi sasa, askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameshaua shahidi watoto 1,335 wa Kipalestina tokea mwaka wa 2000.
Ripoti hiyo imesema kuwa, watoto wa Kipalestina wameuawa shahidi katika matukio ya ufyatuaji risasi, uvurumishaji wa maroketi na mabomu katika uvamizi wa Wazayuni kwenye ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Umoja wa Mataifa umenukuu Wizara ya Afya ya Palestina ikisema kuwa, watoto 15 wa Kipalestina wameuawa shahidi tokea mwanzoni mwa mwaka huu wa 2011 katika Ukanda wa Ghaza pekee, ambapo watatu kati yao waliuawa shahidi walipokuwa wakicheza nje ya nyumba zao.
Jumatano iliyopita, watoto watatu wa Kipalestina wamejeruhiwa na mabaki ya silaha za utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyoripuka katika Ukanda wa Ghaza.
Hilo lilikua tukio jingine ambapo mabaki ya zana za kivita yaliyoachwa katika mashambulizi yaliyoanzishwa na Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza yanaendelea kuwadhuru wakazi wa eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment