BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UMOJA WA MATAIFA WATAKA MAREKENI ITOE MAELEZO JUU YA KIFO CHA OSALAMA BI LADEN.


PICHA ZA PAMOJA ZA KUTENGENEZA KATI YA RAIS OBAMA NA OSAMA.


Umoja wa Mataifa wataka Marekani itoe maelezo kuhusu kuuawa Bin Laden
Marekani imetakiwa na Umoja wa Mataifa itoe maelezo kamili kuhusu kuuawa kinara wa kundi la Al Qaeda Osama bin Laden.

Wajumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Christof Heyns anayeshughulikia mauaji yaliyo kinyume cha sheria na Martin Scheinin anayehusika na kulinda haki za binadamu wakati wa kupambana na ugaidi wamesema wanataka kujua iwapo haki za binaadamu zilizingatiwa wakati wa hujuma iliyopelekea kuuawa Bin Laden.

Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wanasema kuwa ni muhimu kufahamu ikiwa mipango ya kumsaka Osama ilitoa nafasi ya kumkamata. Prof Heyns anasema kuwa hata kama matumizi ya nguvu yanaweza kuruhusiwa ili kulinda maisha magaidi wanastahili kuchukuliwa kama wahalifu kwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Marekani imesema wakati Bin Laden alipouawa wiki iliyopita nchini Pakistan hakuwa na silaha. Rais Barack Obama wa Marekani amezuia kuonyeshwa picha za maiti ya kiongozi wa mtandao wa al Qaida Usama bin Laden huku kukiwepo mjadala mkubwa katika uga wa kimataifa juu ya jinsi kiongozi huyo alivyouawa na taathira zake katika medani ya kimataifa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: