BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHEKA AKIJIANDAA KUMTWANGA KONDE WANYONYI.



FRANCIS CHEKA KULIA AKIJIANDAA KUMTWA KONDE DANIEL WANYONYI AMBALO LILIMPELEKA CHINI KATIKA PICHA INAYOFUATA AMBAPO CHEKA ASHINDA KWA POINTI 100-95, 100-93, 100-93.


WANAMASUMBWI nguli nchini Tanzania wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka (SMG) ameendelea kuonyesha umwamba wake baada ya kumtwanga bondia wa Kenya, Daniel Wanyonyi katika mpambano wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.


Mpambano huo ulioshuhudiwa na maelfu ya washabiki wa mchezo huo kutoka mkoani Morogoro na mikoa jirani ulimalizika baada ya Cheka kuibuka na ushindi wa jumla ya pointi 100-95 alizopata Mkenya huyo.
Katika mpambano huo wa raundi 10 ulianza kwa bondia Francis Cheka kumrushia makonde mazito ya haraka haraka mpinzani wake katika raundi ya kwanza huku akitaka kumaliza mchezo huo mapema lakini Wanyonyi mwenye wajihi wa upole aliweza kuhimili makonde hayo.


Hata hivyo bondia Wanyonyi alionyesha kuzidiwa katika raundi ya pili, tatu tano na saba lakini katika raundi ya nne, sita, nane na kumi aliweza kuonyesha uhai kwa kujibu mapigo na kutaka kuonyesha kuwa yeye pia ni bondia mahili.


kwenye raundi ya nane na tisa Wanyonyi aliweza kudondoka chini mara mbili baada ya kung'utwa ngumi nzito na Cheka lakini aliweza kunyanyuka chini na kuendelea na mchezo huo ambao ulichezeshwa na mwamuzi Omari Yazidu wa Dar es Salaam.



Kutokana na tathimini iliyotolewa na majaji wote watatu wa mchezo huo walimpa Cheka pointi 100, huku majiji hao wakitofautiana kwa ambapo Ibarahim Kamwe alimpa alama 95, Omari Yazidu alitoa poitni 93 na Kondo Nassoro akimpa pointi 93 huku Cheka akipata pointi 100 kutoka kwa majaji hao.

Aidha mpambano huo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa ulitanguliwa na mapambano matatu ambapo katika pambano la kwanza Ramadhan Mkundi wa Dar es Salaam alishinda Juma Afande wa Morogoro kwa pointi 60-54


Mpambano mwingine wa utangulizi ulimshuhudia Bakari Mhomeji wa Dar es Salaam na Seba Temba wa Morogoro kutoka suluhu ya TKD, huku Allan Kamote wa Tanga na Deo Njiku wa Morogoro walitoka suruhu ya pointi 39-39.


Bondia Francis Cheka ambaye anashikilia mikanda ya ICB, WBO na UBO amepigana mapambo 32 huku akiwa ameshinda mapambano 15 kwa KO huku akishinda kwa pointi tisa akipoteza sita na kutoa sare mawili wakati kwa bondia Daniel Wanyonyi yeye akishinda amepigana mapambano 14 akiwa ameshinda kwa KO 10, pointi nne akipoteza matatu na kutoa sare sita.
SHUKA CHINI PICHA ZINAENDELEA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: