BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHEKA AMTAHADHALISHA DANIEL WANYONYI KATIKA PAMBANO LAO KATIKIA UWANJA WA JAMHURI MKOANI MOROGORO.


Bondia Francis Cheka akiwa nyumbani kwake na wadogo zake, Iddi Shabaan kulia na Salum Kimego huku akiwa na mikanda tofauti aliyoshinda katika mapambano mbalimbali aliwahi kucheza.


BONDIA Francis Cheka SMG wa Tanzania mwenye kazi yake mkoani Morogoro amemtahadhalisha mpinzani wake kutoka nchini Kenye bondia Daniel Wanyoni kuwa makini katika pambano lao la kirafiki la ngumi za kulipwa kuwa kwani amepania kumtwanga mapema katika pambano hilo dhidi yake ambalo litakalofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Cheka ambeya anashikilia mikanda ya ICB, WBO na UBO amemtahadhalisha bondia Daniel Wanyonyi kuwa makini muda wote wa pambano hilo kwani amepania kumaliza pambano hilo mapema kwani pambano hilo litakuwa mazoezi tosha kwa ajili ya kujindaa na pambano dhidi ya Mada Maugo ambalo litafanyika mapema septemba mwaka huu.

Kauli hiyo ya bondia Cheka imekuja baada ya mpinzani wake huyo kujigamba kuwa amekuja Tanzania kwa lengo la kuondoka na ushindi katika pambano hilo na kuwapata zawadi wakenya.

“nafahamu kuwa huyu jamaa ni mzuri kutokana na waandaji kufahamu sifa zangu hivyo wasingeweza kuniletea mpinzani ambaye hana uwezo wa kuzichapa na bondia bora kwa Tanzania hivi sasa”. Alisema Cheka.

Alisema kuwa nami nahitaji kuwa makini katika pambano hilo ili kuwapata zawadi mashabiki wangu wa Morogoro na Tanzania kiujumla kwani nisingependi kuwaangusha katika pambano hilo na ikitokea kupoteza mchezo sio malengo yangu.

Bondia huyo ambaye muda mwingi amekuwa akifanya mazoezi katika gym ya Simba Oli na nyumbani kwake mtaa wa Kilimahema Manispaa ya Morogoro amelichukulia pambano hilo kama maandalizi tosha kwa ajili ya kuvaana na bondia Mada Maugo atajitahidi kushinda ili kuendeleza rekodi ya kuwashinda wapinzani wake.

Akielezea juu ya mchezo huo dhidi ya mpinzani wake Cheka alisema kuwa ngumi ni kazi yake ambayo inamuingizia kipata hivyo suala la kupoteza mchezo ni sehemu ya matokeo ya mchezo hivyo asingependi kupoteza pambano hilo kwani atalamizika kuwa makini zaidi katika pambano hilo.

Mchezo huo ni wamakosa hivyo ukifanya kosa utaweza kupoteza kwa hali hiyo imewahi kuwatokea mabondia wakubwa kama bondia Mohamed Ally, Amir Khan na Lowis walitamba katika mchezo huo.

Kwa mujibu bondia huyo Francis Cheka katika mahijiano hayo yalifanyika nyumbani kwake Kilimahema alibanisha kuwa amecheza mapambano 40 kati yao ni mambano 31 ndiyo yaliyorekodiwa huku akishinda mapambano 15 kwa KO, mapambano nane akishinda kwa pointi, sita akiwa amepoteza na mapambano mawili akiwa ametoa sare.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: