BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UMITASHUMTA NGZI YA MKOA MOROGORO YAFIKIA TAMATI BAADA YA KUMALIZIKA KWA MICHEZO YA FAINALI JAMHURI 2011.

MASHINDONO ya umoja wa michezo shule za msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya mkoa wa Morogoro yamefikia tamati mara baada ya kumalizika kwa michezo mitatu tofauti ya fainali kwa kupata mabingwa katika michezo hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Akizungumza na wanamichezo wakati wa kufunga mashindano hayo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Mratibu wa Umitashumta ngazi ya mkoa wa Morogoro Neema Msita alisema mashindano ya michezo hiyo yamefikia tamati mara baada ya kumalizika kwa michezo mitatu tofauti ya fainali kwa mwaka 2011.

Msita alisema kuwa katika mchezo wa soka kwa wavulana timu ya Kilosa imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuitandika timu ya Kilombero kwa kuifunga kwa bao1-0 lililofungwa na mshambuliaji Salum Chawatemi katika kufuatia pasi ya Hemed Mtambo katika mchezo huo.

Katika mchezo wa netiboli Mratibu huyo alisema kuwa timu ya Morogoro Manispaa nayo ilifanikiwa kutwaa ubingwa kwa mchezo wa fainali dhidi ya wilaya ya Mvomero kwa kukubali kipigo cha mabao 27-10.

Alisema mchezo wa wavu wasichana Morogoro Manispaa iliweza kuibuka na ubingwa katika mchezo kwa kuwafunga timu ya wilaya ya Mvomero kwa seti 2-0.

Huku katika fainali ya mchezo wa kuruka juu wavulana Kapaston Rombo kutoka wilaya ya Kilosa alifanikiwa kuibuka bingwa kwa upande wa mchezo huo baada ya kuruka juu kwa umbali wa sentimita 135 huku upande wa wasichana Maria Semwako Mvomero alifanikiwa naye kuibuka na ubingwa kwa wasichana kwa kuruka juu kwa sentimeta 125.

Katika mashindano hayo ya UMITASHUTA ngazi ya mkoa huo ilishirikisha wilaya sita za mkoa huo yakiwa na lengo la kuchangua wachezaji wataunda timu za michezo tofauti kwa mkoa huo wa Morogoro kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kanda ya mashariki yatayofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: